Dini ikitawaliwa na siasa ndo basi tena .. Eid imesetiwa na Kalenda kuwa ni jumamosi (Kalenda Ya 2023) ila kalenda ya kiislam (1 tarehe moja mwezi wa 10 ndo Eid ) sasa Waislamu wa Tanzania sijui wanafuata ukristo au ni gani sielewi.
Tangia Yesu aondoke Duniani... ni miaka 2023 mpaka sasa na waislamu wanatumia kalenda ya kikristo wakidai wao ni waislamu.. inafikirisha sana.
Ndo maana nishawai kusema kuwa mwanzilishi wa dini hizi kuwa na majina ni wakristo maana utaratibu bado tunatumia ule ule....
Hayo mengine hayanihusu ila nachojua kesho lodge zitajaa,pombe zitanywewa za kutosha,night club zitajaa,bila kusahau mauzo ya mdudu kesho yatatia fola.
Dini zote zipo chini ya siasa. Ukibisha anagalia usajili ni kielelezo tosha. Hakuna mwanadini anayekohoa mbele ya mwanasiasa. Siasa inaitumia dini kutawala raia. Utasikia viongozi wa dini wakiwakingia kifua wanasiasa wasiguswe wamewekwa na mungu tii mamlaka toka kwa mungu.