Leo katika historia: Jenerali Mstaafu David Musuguri alizaliwa Januari 4, 1920. Atimiza miaka 102

Iwaay

Member
Joined
May 21, 2016
Posts
36
Reaction score
56
Jenerali mstaafu David Bugozi Waryoba Musuguri alizaliwa Januari 4, ‌1920 katika Kijiji cha Kumuruti, Masabha. Sasa sehemu hiyo inajulikana kama Nyasirori, akiwa mtoto wa tatu katika familia ya mzee Musuguri wa Nzangho.

Alipozaliwa aliitwa jina la Waryoba, ikiwa ni ishara kwamba alizaliwa asubuhi wakati jua linachomoza. Baba yake mkubwa, Mgendi wa Nzangho alimwita jina la Bugingo.

Akiwa na umri wa miaka mitano, mzee Musuguri Nzangho alihamia Kijiji cha Butiama‌, ‌wakati huo paliitwa ‌Mu-kyaro.

Jenerali mstaafu David Bugozi Waryoba Musuguri alikuwa mtoto wa tatu kuzaliwa katika tumbo la mama yake, Wakuru wa Kibumbiko. Bibi mzaa mama yake pia alikuwa anaitwa Wakuru wa Kigeso. Jina la Wakuru ni jina kubwa sana katika ukoo huu wa Jenerali Musuguri.

Mzee Musuguri wa Nzangho alioa wanawake ‌sita. Alikuwa mfugaji wa ng’ombe na mbuzi na alikuwa stadi kulinda mifugo yake, kwani yeye na wachungaji wenziwe waliwahi kwenda kuwinda simba na waliua simba 18‌.

Enzi hizo wanyama wa pori walikuwa wapo mapori ya karibu maeneo ya ‌Bisarye, Ikizu na Buhemba.

Akiwa kijana mdogo, hakubahatika kwenda shule. Muda mwingi alichunga ng’ombe na mbuzi wa baba yake, kwa kuwa alikuwa mtoto wa kiume pekee hapo kwao, wengine walikuwa wasichana.

Jina la Bugozi

Jenerali Musuguri kwa maisha yake ya kazi amejulikana pia kwa jina la Bugozi. Jina hili alijiita mwenyewe kutokana na uwezo wake wa kupigana mieleka, inayojulikana kwa Kizanaki kama, ‘erigori.’ Wakati huo ‘erigori‌’ lilifanyika eneo ambalo lilipata umaarufu kwa kuitwa jina lake hilo.

Kuingia Jeshi la Mkoloni – King’s African Rifles (KAR)

Jenerali Musuguri aliingia jeshini ‌katika mazingira tata. Mwenyewe anasimulia kwamba kati ya mwaka 1942 au 19‌43, katika sehemu ya kilima cha Mutuzu‌, ‌Butiama kuna mama aliuawa kutokana na sababu za kishirikina. Polisi walifika ‌hapo kijijini na kuwakamata vijana ili wasaidie kubeba mwili wa marehemu ‌kuupeleka Musoma kwa ajili ya uchunguzi.

Wakati wakisubiri kwenda Musoma‌, ‌waliwekwa rumande kwenye boma la Chifu Edward Wanzagi Nyerere. Lakini usiku kabla ya safari hiyo‌, ‌kijana Waryoba Musuguri akiwa na umri wa miaka 22, na vijana wengine walitoroka na kwenda Musoma‌. Huko akajiandikisha kujiunga katika Jeshi la KAR.

Alipotoroka aliambatana na wenzake – ‌Mugendi Nyamatwema na Mkono wa Nzenzere. Wakatembea mpaka Musoma kujiunga jeshini.

Wakati huo Chifu Edward Wanzagi Nyerere alikuwa ametawazwa mwaka 1942 baada ya baba yake, Chifu Nyerere Burito, kufariki dunia.

Baadaye alijiunga na vijana wenziwe Mwanza, wengine wakajiunga Morogoro, mpaka walipo‌fika ‘depo’ ya mafunzo Dar es Salaam.

Akiwa jeshini ndiko alikopata elimu ya kusoma na kuandika, na akaweza kujiendeleza hata kufanya kozi ‌mbalimbali za kijeshi katika nchi za Canada na China.

Akiwa KAR alipigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia ambayo ilimwezesha kupigana katika uwanja wa vita katika nchi nyingi, zikiwamo India, Burma, Ushelisheli, Canada, mpaka Japan ambako alijeruhiwa kwa risasi kwenye paja. Alivuja damu na kupoteza ‌fahamu‌. Alibebwa na askari mwingine Mtanzania aliyeitwa Marega – huyu anatoka Ngoreme. Kwa kitendo hicho cha kumwokoa, aliendelea ‌kuwa rafiki yake wa karibu hadi alipofariki dunia.

Akiwa KAR‌, miongoni mwa wanafaunzi wake ni aliyekuja kuwa kiongozi wa Uganda, ‌Idd Amin Dada, aliyejiunga na jeshi la KAR, Kahawa Barracks mjini Nairobi.

Jenerali ‌Musuguri pia alipigana vita ya MAUMAU nchini Kenya baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia akiwa jeshi la KAR.

Mwaka 1957 aliongoza kikosi cha wanajeshi wa KAR kutoka Afrika Mashariki kwenda London, Uingereza kwenye gwaride la Malkia wa Uingereza. Alipeleka ‌historia ya KAR katika Afrika Mashariki, na yeye ndiye aliyemkabidhi historia hiyo Malkia Elizabeth II Juni 11, 1957 katika Kasiri la Mfalme la Buckingham wakati huo akiwa na cheo cha Warrant Officer Platoon Commander (W.O.P.C). Alikuwa Mwafrika wa kwanza kuonana na kupeana mkono na Malkia Elizabeth II wa Uingereza.Uhuru

Baada ya Uhuru wa Tanganyika Desemba 9, 1961, aliendelea kuwapo jeshini. Baada ya Uhuru KAR ilibadilishwa jina na kuitwa Tanganyika Rifles.

Baada ya maasi ya mwaka 1964, Jeshi la Tanzania liliundwa upya likawa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ‌) ‌au Tanzania People’s Defence Forces (TPDF)‌, ‌likiwa na viongozi Watanzania wazalendo. Alikwenda kwenye vita ya Kagera ya kumtimua nduli Idd Amin ‌kati ya mwaka 1978 hadi 1979, ambako alitambulika kwa kuongoza vita kishupavu na akaitwa ‘‌Jenerali Mutukula, ‌Kamanda mwenye Uso wa Chuma’.

Jenerali mstaafu ‌Musuguri alipitia vyeo vyote vya kijeshi kuanzia ‘Private’ mpaka ‘‌Full General’ akiwa Mtanzania wa kwanza kupata cheo hicho cha ‘‌Full General’.

Aliendelea kufanya kazi ya jeshi kwa weledi na ujasiri hadi alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ‌(CDF). Kwa mtiririko wa ma-‌CDF wa JWTZ, Jenerali Musuguri alikuwa ‌wa tatu.

Alistaafu kazi ya jeshi mwaka 1988 na tangu hapo amekuwa akiishi nyumbani kwake Butiama (‌Makao Makuu ya

Wilaya ya Butiama) akijishughulisha na kilimo na ufugaji.

Baada ya kustaafu‌, ‌Jenerali mstaafu David Bugozi Waryoba Musuguri, akiwa kijijini alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Butiama, mwaka 1990 hadi mwaka 1991.

Katika siku hii ya leo (Januari 4, 2022 ‌Jenerali Mutukula anatimiza umri wa miaka 102.
Screenshot_20220104-141947.jpg
 
..Mtanzania wa kwanza kupewa rank ya Jenerali ni Abdalah Twalipo, jina la kivita " Jenerali chakaza. "

..Abdalah Twalipo alikuwa Mkuu wa majeshi / Cdf wa pili tangu JWTZ ilipoanzishwa mwaka 1964. Pia alikuwa mkuu wa majeshi wakati wa vita vya Kagera.

..Wakati Mwalimu Nyerere anakaribia kustaafu alitoa nishani kwa watu mbalimbali na pia aliwapa rank ya Jenerali / full general askari wawili.

..Luteni Jenerali Abdalah Twalipo alikuwa wa kwanza kuvikwa cheo chake na Rais Nyerere.

..Baada ya Twalipo, Rais Nyerere alimvika Luteni Jenerali David Musuguri cheo cha Jenerali.

..Vita vya Kagera / Uganda vilipiganwa kwa " awamu mbili ."

..Awamu ya kwanza ilipiganwa ktk ardhi ya Tanzania na ilihusisha zoezi la kuyafukuza majeshi ya Uganda kutoka ktk mipaka yetu.

..Awamu ya pili ilihusisha mapigano ndani ya ardhi ya Uganda kwani Amin pamoja na kuwa ameondolewa ktk ardhi yetu akiendelea kutishia kurudi na alikuwa akituma ndege za kivita kutushambulia.

kila awamu ilikuwa na kamanda wake mkuu ambaye alikuwa na makamanda wengine chini yake.

..David Musuguri [ akiwa meja jenerali] alikuwa kamanda mkuu wa majeshi ya Tanzania yaliyoingia Uganda kumfukuza Idi Amin na majeshi yake.

..Baada ya vita vya Kagera / Uganda Musuguri alipandishwa cheo kuwa Luteni Jenerali na kuteuliwa kuwa mkuu wa majeshi / Cdf akimpokea nafasi hiyo Abdalah Twalipo.

NB.

..Abdalah Twalipo ndio Mtanzania wa kwanza kupewa rank ya General.

..David Musuguri ndio CDF / mkuu wa majeshi wa kwanza kutumikia ktk nafasi hiyo akiwa na cheo cha General.
 
Amekula chumvi ya kutosha, baba yangu alizaliwa 1922 na mama 1923 lakini wote waliishaenda Mbinguni.

Huwa naona kama upo umri ukifikia unakuwa hauna tena furaha.
 
Jenerali mstaafu David Bugozi Waryoba Musuguri alizaliwa Januari 4, ‌1920 katika Kijiji cha Kumuruti, Masabha. Sasa sehemu hiyo inajulikana kama Nyasirori, akiwa mtoto wa tatu katika familia ya mzee Musuguri wa Nzangho.

Alipozaliwa aliitwa jina la Waryoba, ikiwa ni ishara kwamba alizaliwa asubuhi wakati jua linachomoza. Baba yake mkubwa, Mgendi wa Nzangho alimwita jina la Bugingo.

Akiwa na umri wa miaka mitano, mzee Musuguri Nzangho alihamia Kijiji cha Butiama‌, ‌wakati huo paliitwa ‌Mu-kyaro.

Jenerali mstaafu David Bugozi Waryoba Musuguri alikuwa mtoto wa tatu kuzaliwa katika tumbo la mama yake, Wakuru wa Kibumbiko. Bibi mzaa mama yake pia alikuwa anaitwa Wakuru wa Kigeso. Jina la Wakuru ni jina kubwa sana katika ukoo huu wa Jenerali Musuguri.

Mzee Musuguri wa Nzangho alioa wanawake ‌sita. Alikuwa mfugaji wa ng’ombe na mbuzi na alikuwa stadi kulinda mifugo yake, kwani yeye na wachungaji wenziwe waliwahi kwenda kuwinda simba na waliua simba 18‌.

Enzi hizo wanyama wa pori walikuwa wapo mapori ya karibu maeneo ya ‌Bisarye, Ikizu na Buhemba.

Akiwa kijana mdogo, hakubahatika kwenda shule. Muda mwingi alichunga ng’ombe na mbuzi wa baba yake, kwa kuwa alikuwa mtoto wa kiume pekee hapo kwao, wengine walikuwa wasichana.

Jina la Bugozi

Jenerali Musuguri kwa maisha yake ya kazi amejulikana pia kwa jina la Bugozi. Jina hili alijiita mwenyewe kutokana na uwezo wake wa kupigana mieleka, inayojulikana kwa Kizanaki kama, ‘erigori.’ Wakati huo ‘erigori‌’ lilifanyika eneo ambalo lilipata umaarufu kwa kuitwa jina lake hilo.

Kuingia Jeshi la Mkoloni – King’s African Rifles (KAR)

Jenerali Musuguri aliingia jeshini ‌katika mazingira tata. Mwenyewe anasimulia kwamba kati ya mwaka 1942 au 19‌43, katika sehemu ya kilima cha Mutuzu‌, ‌Butiama kuna mama aliuawa kutokana na sababu za kishirikina. Polisi walifika ‌hapo kijijini na kuwakamata vijana ili wasaidie kubeba mwili wa marehemu ‌kuupeleka Musoma kwa ajili ya uchunguzi.

Wakati wakisubiri kwenda Musoma‌, ‌waliwekwa rumande kwenye boma la Chifu Edward Wanzagi Nyerere. Lakini usiku kabla ya safari hiyo‌, ‌kijana Waryoba Musuguri akiwa na umri wa miaka 22, na vijana wengine walitoroka na kwenda Musoma‌. Huko akajiandikisha kujiunga katika Jeshi la KAR.

Alipotoroka aliambatana na wenzake – ‌Mugendi Nyamatwema na Mkono wa Nzenzere. Wakatembea mpaka Musoma kujiunga jeshini.

Wakati huo Chifu Edward Wanzagi Nyerere alikuwa ametawazwa mwaka 1942 baada ya baba yake, Chifu Nyerere Burito, kufariki dunia.

Baadaye alijiunga na vijana wenziwe Mwanza, wengine wakajiunga Morogoro, mpaka walipo‌fika ‘depo’ ya mafunzo Dar es Salaam.

Akiwa jeshini ndiko alikopata elimu ya kusoma na kuandika, na akaweza kujiendeleza hata kufanya kozi ‌mbalimbali za kijeshi katika nchi za Canada na China.

Akiwa KAR alipigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia ambayo ilimwezesha kupigana katika uwanja wa vita katika nchi nyingi, zikiwamo India, Burma, Ushelisheli, Canada, mpaka Japan ambako alijeruhiwa kwa risasi kwenye paja. Alivuja damu na kupoteza ‌fahamu‌. Alibebwa na askari mwingine Mtanzania aliyeitwa Marega – huyu anatoka Ngoreme. Kwa kitendo hicho cha kumwokoa, aliendelea ‌kuwa rafiki yake wa karibu hadi alipofariki dunia.

Akiwa KAR‌, miongoni mwa wanafaunzi wake ni aliyekuja kuwa kiongozi wa Uganda, ‌Idd Amin Dada, aliyejiunga na jeshi la KAR, Kahawa Barracks mjini Nairobi.

Jenerali ‌Musuguri pia alipigana vita ya MAUMAU nchini Kenya baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia akiwa jeshi la KAR.

Mwaka 1957 aliongoza kikosi cha wanajeshi wa KAR kutoka Afrika Mashariki kwenda London, Uingereza kwenye gwaride la Malkia wa Uingereza. Alipeleka ‌historia ya KAR katika Afrika Mashariki, na yeye ndiye aliyemkabidhi historia hiyo Malkia Elizabeth II Juni 11, 1957 katika Kasiri la Mfalme la Buckingham wakati huo akiwa na cheo cha Warrant Officer Platoon Commander (W.O.P.C). Alikuwa Mwafrika wa kwanza kuonana na kupeana mkono na Malkia Elizabeth II wa Uingereza.Uhuru

Baada ya Uhuru wa Tanganyika Desemba 9, 1961, aliendelea kuwapo jeshini. Baada ya Uhuru KAR ilibadilishwa jina na kuitwa Tanganyika Rifles.

Baada ya maasi ya mwaka 1964, Jeshi la Tanzania liliundwa upya likawa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ‌) ‌au Tanzania People’s Defence Forces (TPDF)‌, ‌likiwa na viongozi Watanzania wazalendo. Alikwenda kwenye vita ya Kagera ya kumtimua nduli Idd Amin ‌kati ya mwaka 1978 hadi 1979, ambako alitambulika kwa kuongoza vita kishupavu na akaitwa ‘‌Jenerali Mutukula, ‌Kamanda mwenye Uso wa Chuma’.

Jenerali mstaafu ‌Musuguri alipitia vyeo vyote vya kijeshi kuanzia ‘Private’ mpaka ‘‌Full General’ akiwa Mtanzania wa kwanza kupata cheo hicho cha ‘‌Full General’.

Aliendelea kufanya kazi ya jeshi kwa weledi na ujasiri hadi alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ‌(CDF). Kwa mtiririko wa ma-‌CDF wa JWTZ, Jenerali Musuguri alikuwa ‌wa tatu.

Alistaafu kazi ya jeshi mwaka 1988 na tangu hapo amekuwa akiishi nyumbani kwake Butiama (‌Makao Makuu ya

Wilaya ya Butiama) akijishughulisha na kilimo na ufugaji.

Baada ya kustaafu‌, ‌Jenerali mstaafu David Bugozi Waryoba Musuguri, akiwa kijijini alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Butiama, mwaka 1990 hadi mwaka 1991.

Katika siku hii ya leo (Januari 4, 2022 ‌Jenerali Mutukula anatimiza umri wa miaka 102. View attachment 2068256
Ni baraka kubwa kuona mTz aliyekula chumvi hivi. Nafahamu vijana na wadada kadhaa wameshatangulia na hata miaka 20 walikuwa hawajafikisha 😭😭😭
 
Ubarikiwe sana mkuu kwa hii historia,umesema mengi na umesema kweli,natamani niseme zaidi.
 
  • Thanks
Reactions: MCN
Namtakia.maisha marrfu Generali musuguli.hakika maisha yake ni zawadi kwa watanzania na kwa alivyo mkakamavu naamini mungu amekusudia kumpa maisha marefu zaidi. Hbd General
 
Na sisi wenye kituo chetu pendwa hapa Mbezi "nishushe kwa Musuguri" tuseme ndio asili ya jina la General Musuguri?
 
Back
Top Bottom