Leo katika historia Tanganyika

Leo katika historia Tanganyika

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Hii ndio ilikuwa Bendera yetu, na katikati ya Bendera ni Ngao ya Jamii (Coat of Arms) ya Nchi yetu enzi tunaitwa Deutsch-Ostafrika (Ujerumani ya Afrika Mashariki) miaka ya 1885 mpaka 1918.

Wakati huo nchi ilikuwa na eneo la Mita Square 994,996 Km² ndani yake kuna Burundi na Rwanda, na Eneo la Nchi ya Msumbiji lililoitwa Kionga Triangle.

Je wajua neno la Kiswahili "Shule" limetoka kwenye Neno la Kijerumani "Schule" yote yakimaanisha "School".

Maeneo mengine yaliitwa hivi:

• Rombo iliitwa Fischerstadt
• Nyakanazi iliitwa Friedberg
• Kisarawe iliitwa Hoffnungshöh
• Tukuyu iliitwa Langenburg
• Ushetu iliitwa Marienthal
• Shume (huko kwa Wapare wambugu) kuliitwa Neu-Hornow
• Mbulu kuliitwa Neu-Trier
• Sekenke paliitwa Sachsenwald na ilikua ni Mgodi.
• Lushoto iliitwa Wilhelmsdorf.

Kipindi hiki ndio tulijengewa Reli iliyoitwa Usambara Railway mwaka 1891 ilijengwa na Wajerumani na ilikuwa na Km 350, ilianzia Mjini Tanga, ikawa na makutano na Kenya Mji wa Kahe, ikapita Moshi mpaka Arusha.

Wajerumani katika Reli hii walikuwa na vichwa vya Treni 18 (Locomotive) na mabehewa 199, kipindi hicho Reli hii ilikuwa na wafanyakazi 562 huku kati yao 35 tu ndio walikuwa Wajerumani.

Lengo la Wajerumani kujenga Reli hii ilikuwa ni kuunganisha Bandari ya Tanga na Ziwa Victoria kupitia milima ya Usambara.

Treni la kwanza lilipita likiwa tupu tarehe 26 September 1911 ili kujaribu safari na kufanikiwa 100%, likapita tena likiwa na Abiria tarehe 4 October 1911 na kufanikiwa 100% Wajerumani wakaamini kweli kitu ni Konki.

Hivyo ukafanyika uzinduzi wa Reli tarehe 7 February 1912, na baada ya hapo Treni lilikuwa lazima lifanye safari kila siku kutoka Tanga mpaka Buiko na Kurudi, safari ilichukua muda wa masaa 14 na dakika 40.

Reli hii haikukamilika mpaka Arusha sababu ya Vita ya kwanza ya Dunia, Waingereza ndio Wakaiunganisha.

#Kutoka_Maktaba
FB_IMG_1735523953191.jpg
 
Mungu ibariki Tanganyika!
Ephemeral Evolution ... 🤍 ...
As the sands of time flow and another year begins, 'Ephemeral Evolution' invites us to reflect on the beauty of transformation. Like the butterfly emerging from its chrysalis, the New Year brings an opportunity to embrace growth, hope, and the delicate yet powerful nature of change.
Tanganyika ❤📌🔨💪🏿
FB_IMG_1735526157756.jpg
 
Hii ndio ilikuwa Bendera yetu, na katikati ya Bendera ni Ngao ya Jamii (Coat of Arms) ya Nchi yetu enzi tunaitwa Deutsch-Ostafrika (Ujerumani ya Afrika Mashariki) miaka ya 1885 mpaka 1918.

Wakati huo nchi ilikuwa na eneo la Mita Square 994,996 Km² ndani yake kuna Burundi na Rwanda, na Eneo la Nchi ya Msumbiji lililoitwa Kionga Triangle.

Je wajua neno la Kiswahili "Shule" limetoka kwenye Neno la Kijerumani "Schule" yote yakimaanisha "School".

Maeneo mengine yaliitwa hivi:

• Rombo iliitwa Fischerstadt
• Nyakanazi iliitwa Friedberg
• Kisarawe iliitwa Hoffnungshöh
• Tukuyu iliitwa Langenburg
• Ushetu iliitwa Marienthal
• Shume (huko kwa Wapare wambugu) kuliitwa Neu-Hornow
• Mbulu kuliitwa Neu-Trier
• Sekenke paliitwa Sachsenwald na ilikua ni Mgodi.
• Lushoto iliitwa Wilhelmsdorf.

Kipindi hiki ndio tulijengewa Reli iliyoitwa Usambara Railway mwaka 1891 ilijengwa na Wajerumani na ilikuwa na Km 350, ilianzia Mjini Tanga, ikawa na makutano na Kenya Mji wa Kahe, ikapita Moshi mpaka Arusha.

Wajerumani katika Reli hii walikuwa na vichwa vya Treni 18 (Locomotive) na mabehewa 199, kipindi hicho Reli hii ilikuwa na wafanyakazi 562 huku kati yao 35 tu ndio walikuwa Wajerumani.

Lengo la Wajerumani kujenga Reli hii ilikuwa ni kuunganisha Bandari ya Tanga na Ziwa Victoria kupitia milima ya Usambara.

Treni la kwanza lilipita likiwa tupu tarehe 26 September 1911 ili kujaribu safari na kufanikiwa 100%, likapita tena likiwa na Abiria tarehe 4 October 1911 na kufanikiwa 100% Wajerumani wakaamini kweli kitu ni Konki.

Hivyo ukafanyika uzinduzi wa Reli tarehe 7 February 1912, na baada ya hapo Treni lilikuwa lazima lifanye safari kila siku kutoka Tanga mpaka Buiko na Kurudi, safari ilichukua muda wa masaa 14 na dakika 40.

Reli hii haikukamilika mpaka Arusha sababu ya Vita ya kwanza ya Dunia, Waingereza ndio Wakaiunganisha.

#Kutoka_MaktabaView attachment 3188252
Siku hizi, Huko mashuleni huwezi kuipata tena historia hii.
 
Historia haiongopi.. Naamini kuna siku Tanganyika itarejea
Bila shaka Tanganyika (Afrika mashariki ya ujerumani )uliyoileta kwenye mada haiwezi kurudi! Kwa sababu italazimika kuyafuta mataifa ya Rwanda na Burundi na sehemu ya nchi ya Mosambique kama ulivyotaja na hilo siyo rahisi kutokea.
Majadiliano yakienda vizuri yawezekana kurudisha Tanganyika ya mwingereza hadi kabla ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar na hilo litawezekana endapo tutakuwa tayari kuvunja muungano kila upande uangalie mambo yake au tukubali muungano wa serikali tatu.
 
Back
Top Bottom