Leo kutatokea ' Nyuki ' wengi Uwanja wa Mkapa ( Taifa ) kuanzia Saa 5 asubuhi hadi Saa 1 jioni hivyo Watu wasiende hilo eneo kabisa

Leo kutatokea ' Nyuki ' wengi Uwanja wa Mkapa ( Taifa ) kuanzia Saa 5 asubuhi hadi Saa 1 jioni hivyo Watu wasiende hilo eneo kabisa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Usije kusema sijakuambia kwani hao Nyuki ni wale wa Kuja na Kasi ya Upepo kutoka Bahari ya Hindi ambao ni wakali sana na wanaweza Kukuachia Nundu nyingi Kichwani na hata Mwilini kwako. Hata hivyo Nyuki hao ikifika tu Saa 1 Usiku wataondoka hilo eneo na Kutokomea zao kabisa.

Njia pekee ya Kujikinga na hao Nyuki kwa mtakaokwenda Uwanjani hapo au eneo la Uwanja wa Mkapa ni Kuvalia ama Nguo za Rangi Nyeupe na Nyekundu tu ila Kitaalam hawa Nyuki wakikuona Umevalia Nguo zenye Rangi ya Kijani au Njano ndiyo utawapandisha Hasira na ' Watakung'ata ' vibaya mno na Kupelekea Kuvimba.

Na usije Ukajiroga leo hii uende Temeke huku sijui ukiwa umevalia Pensi ( Vinjunga ) kwani hawa Nyuki ndiyo wanaweza hata Kupenya hadi maeneo ' Hatarishi ' ya Mwili wa Binadamu na ambayo ni muhimu pia kwa Ujazaji wa hii dunia. Mtaalam mmoja wa hawa Nyuki wanaotembea na Kasi ya Upepo amesema kuwa kama kuna Kikundi cha Watu leo kinapanga Kutembelea maeneo ya Temeke basi njia pekee ya kuwaepuka hawa Nyuki ni Kuvalia tu hizo Nguo za Rangi Nyeupe au Nyekundu na si Njano au Kijani kwani Kiutaalam Nyuki anazichukia sana hizi rangi.

Akili za Kuambiwa changanya na zako!
 
Natamani kweli mtu apigwe mji utulie..maana wana ngenga kweli..

Ndugu kwani leo kuna Tukio gani hapo Uwanja wa Mkapa / Taifa? Bado nahangaika na kuwazuia hawa Nyuki wanaokuja kwa Kasi ya ajabu sasa wakitokea huku Baharini ambao wanaelekea kwa wale wenye ' Viherehere ' watakaonza Kuonekana hapo Uwanjani kuanzia Saa 5 asubuhi hii. Nashauri kama kuna tukio lolote lile linataka Kufanyika hapo Uwanjani basi lipangiwe kuanzia Saa 6 Usiku hadi Saa 8 Usiku ambapo Nyuki hawa watakuwa wameshasinzia. Kama kuna Watu woowte wale wapo njiani kuelekea Taifa warudi kwani hawa Nyuki hawatanii ila kama wanaweza Kununua Nguo zenye Rangi Nyeupe na Nyekundu kisha wakazivaa basi rukhsa tu kwenda hapo.
 
Back
Top Bottom