Katika shule ya sekondari Muungano,mwalimu Ndamo alikuwa yuko darasani na alikuwa anamalizia kipindi katika somo la Historia,alikuwa anaacha kazi kwa ajili ya wanafunzi kuifanya na ndipo wavulana wawili walinyanyuka katika viti vyao kuelekea mbele ya darasa mahali ambapo mwalimu alikuwepo na waliomba watoke nje ya darasa waende maliwato.
Alisikika mwalimu akisema "Sitowaruhusu mtoke wawili kwenda kwenda maliwato,aende mmoja kwanza"alisema mwalimu Tena kwa ukali.
Mwalimu Ndamo hapendi tabia ya wanafunzi kwenda maliwato wawili au zaidi na alishawaeleza wanafunzi wake kuhusu jambo hili mara nyingi Sana na baadhi ya wanafunzi wake walianza kumwelewa na wengine waliona Kama ni mtu aliyepitwa na wakati na kuwapotezea muda.
Walimu katika shule hii waliazimia katika moja ya vikao vyao kuwa wanatakiwa kuwa macho wakati wote katika masuala ya taaluma na malezi ya wanafunzi wao hasa katika nyakati hizi ambapo vitendo vya ulawiti, ushoga na usagaji vimeshamiri na katika nyakati tofauti tofauti matukio Kama haya yameripotiwa katika shule mbalimbali hivyo walimu wa shule hii waliona wana wajibu wa kusimamia malezi kwa kushirikiana na wazazi wa wanafunzi wao kwakuwa walitambua vyema kuwa peke yao wasingeweza na wala wazazi pekee wasingeweza bali kwa kushirikiana wangeweza.
Siku iliyofuata katika shule ya sekondari Muungano ilikuwa ni siku ya tofauti na siku zingine,Ugeni mkubwa ulitarajiwa kuwasili shuleni hapo kwani hii likuwa ni siku ya uzinduzi wa bweni la wasichana na mradi mkubwa wa maji katika kata ya Muungano na sherehe kubwa ilikuwa inatarajiwa kufanyika shuleni hapo hivyo wazazi na wanakijii kwa ujumla walialikwa kuhudhuria sherehe hiyo,maandalizi yalikamilika ukumbi ulipambwa na ukapambika,vikundi mbalimbali vya burudani viliandaliwa na baada ya muda mchache wageni walianza kuwasili shuleni na mshereheshaji aliwakaribisha ukumbini na ilipofika saa 3:30 asubuhi ngeni rasmi aliwasili shuleni na aliingia ukumbini akiwa ameambatana na wasaidizi wake,Mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge jimbo la Mkomaindo.
Sherehe ilianza rasmi baada ya duwa na sala na kikundi cha burudani cha muziki kilipanda jukwaani na kuanza kutumbuiza,shule hii ilijaaliwa wanafunzi wenye vioaji sana kiasi cha kuwafanya kila mtu ukumbini hapo kujawa na msisimko kwa tungo zilizojaa ubunifu wa hali ya juu zilizokuwa zinawaasa vijana dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya, ulawiti, ushoga na usagaji na ulikuwa ni ujumbe wa wazi ambao kila mtu aliuelewa,muda mfupi baadae aliwatambulisha wageni waalikwa pamoja na meza kuu na akatoa na neno la ukaribisho, na baada ya hapo ratiba ya burudani iliendelea na Sasa kikosi cha ubunifu wa mavazi kiliingia ukumbini na aina mbalimbali za mavazi kwa ajili ya onesho la ubunifu wa mavazi,vijana hawa walibuni mavazi kwa kutumia vitu vya kawaida kabisa Kama karatasi za manila,majani ya mgomba, chandarua pamoja na kanga na vitenge,kundi la vijana wavulana kwa wasichana walipita mbele ya Mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa.Ungeweza kudhani mwanamitindo mkubwa Kama Flaviana Matata alikuwepo na aliwapa mwongozo wa nini wakifanye,La hasha,ni kazi ya ubunifu iliyofanywa na wao wenyewe,yaani wanafunzi wa Muungano,kwa mara nyingine tena ukumbi ulilipuka kwa shangwe na nderemo wakati vijana hao walipokuwa wakipita mbele yao,Baadhi ya watu walisikika wakisema "Hawa watoto wako vizuri sana,wana vipawa vya ajabu".
Burudani haikuishia hapo kundi la igizo nalo kiliingia ukumbini,Igizo liliwahusu wasichana wawili ambao walikuwa ni wanafunzi na walikuwa wakitoka umbali mrefu kutoka nyumbani kuelekea shuleni hivyo walilazimika kuamka mapema na hata kabla hakujapambazuka vizuri walianza safari kuelekea shuleni kitu ambacho kilihatarisha usalama wao.
Siku moja Kama kawaida walikuwa wakielekea shuleni ndipo kundi la vijana wapatao tano lilianza kuwakimbiza, wasichana wale walipiga kelele za kuomba msaada huku wakiendelea kuwakimbia vijana hao ambao walionesha dhahiri kuwa walikuwa na nia ovu,sauti zile zilisikiwa na akina baba watatu ambao walikuwa wanamwagilia bustani za mbogamboga asubuhi ya siku hiyo,wakielekea mahali ambako sauti zilisikika,vijana wale walikuwa wameshawazidi mbio wasichana wale na tayari walishawakamata na walikuwa katika purukushani za kutaka kuwabaka lakini kabla hawajafanya kitendo hicho kundi lile la akina baba watatu waliwahi kufika na kuwaokoa na vijana walikimbia lakini baada ya msako mkali na wanakijiji ukiongoza na kamati ya ulinzi ya kijiji kilifanikiwa kuwakamata vijana wale kwakuwa walibainika baada ya siku tatu,na hata uchunguzi ulipofanyika ilibainika kuwa vijana hao hutumia madaya yanjulevya aina ya bangi na hapo walipelekwa kwenye vyombo vya sheria na walihukumiwa kifungo jela.
Mgeni rasmi baadae nae alitoa hotuba watu wote waliokusanyika mahali hapo,katika mengi aliyoyaongea,mojawapo ilikuwa ni kuwasisitiza wanajamii kuhusu kuulinda mradi wa maji na alieleza jinsi bweni ambalo litakavyowasaidia wanafunzi hasa wasichana,alisema" bweni hili ni ukombozi kwenu,Sasa hamtakuwa na hatari yoyote dhidi yenu na mtapata muda mwingi wa kijisomea"
Alieleza zaidi kwa kuwaasa vijana kuachana na matumizi ya mihadarati kwani inafubuza nguvu kazi kwani vijana ndio vyenzo katika ukuaji wa uchumi na hasa ukizingatia kuwa vijana ndio jeshi kubwa.
Aidha mwandishi wa hadithi hii fupi nae anashauri mambo yafuatayo;
Kwanza,Kutambua na kuendeleza vipaji vya watoto kuanzia ngazi ya chini ya ukuaji wa mtoto, na kila mtoto anapobainika kuwa na kipaji fulani basi kipaji hicho kiendelezwe kwakuwa vipaji ni njia mojawapo ya kuondokana na changamoto ya ajira kwakuwa serikali na taasisi binafsi haziwezi kumaliza changamoto ya ajira.
Pili, kazi za sanaa zilenge katika kukemea uovu Kama ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa kingono, wasanii Wana mtaji mkubwa wa watu wanaowafuatilia na kuwaamini hivyo wana nafasi kubwa sana ya kukemea uovu kama wataamua kuelekeza tungo zao huko.
Tatu, Malezi shirikishi ya watoto, jukumu la malezi lisabaki kuwa la mzazi au mlezi pekee bali jamii kwa ujumla ishiriki katika suala la malezi ili kuwa na jamii iliyo na maadili mema,uthabiti wa taifa bora utaletwa na familia bora ,familia bora ndio italeta jamii bora na jamii bora ndio huzaa taifa bora na mataifa yakiwa na ustawi Safi kimaadili basi dunia itabaki kuwa sehemu salama kwa kizazi kilichopo na vijavyo.
Nne, Jamii zetu zifanye kazi kwa bidii na serikali zitumie rasilimali za nchi katika kujenga uchumi imara kwa taifa na kwa mtu mmoja mmoja, Hii itasaidia kuepukana na misaada ya masharti magumu ambayo yanakinzana na mila, desturi, miiko pamoja na utu wetu.
Tano, Nguvu iongezwe katika vita ya mapambano dhidi ya madawa ya kulevya,ongezeko la matumizi ya mihadarati ndio limesababisha kwa kiasi kikubwa vitendo vya ukatili wa kijinsia,ubakaji, ushoga na usagaji,msako wa wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya ufanyike nchi nzima maana hapo ndipo tatizo linapoanzia.
Mwisho, Maadili na uadilifu ndio uwe wimbo wetu,viongozi wa kidini wahuburi bila kuchoka, wazazi na walimu washirikiane na zaidi Tumuombe Mwenyezi Mungu wakati jitihada hizo zikiendelea.
Madudi Mavele.

Upvote
3