RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
💼 MHADHARA NA.4
Wapo wanawake ambao baada ya kuolewa wanaamua kufunga biashara zao halali walizokuwa wakizifanya awali kabla ya kuolewa, kuna ambao wanaamua kuacha kazi, wengine walikuwa mbioni kwenda chuo kusomea ualimu, udaktari, uhasibu, n.k, lakini baada ya kuolewa wanazika ndoto zao.
Leo nakuuma sikio wewe mwanamke; kuolewa kusiwe chanzo cha kuacha kujishughulisha kwenye kazi za kukuingizia kipato hata kama mumeo ameshiba hela. Hata kama umeolewa na tajiri nakushauri kila siku jifunze kuishi bila tajiri. Usibweteke eti kwasababu sikuhizi hupandi tena daladala wala mwendokasi - unapanda BMW, Mercedes-Benz, Bugatti, V8, Prado, Vanguard, n.k - yaani mpaka unasahau kuwa mumeo ana ndugu zake wengi ambao bado hawajatoboa maisha.
Nakukumbusha; siku moja mawifi na mashemeji watakuja na sura ya mbuzi kugawana mali za ndugu yao mbele yako, watakuachia kibanda kimoja tu unachoishi sasa....Bado sikumaliza; wapo wanawake ambao wameolewa na sasa hawawezi tena kulima, kushona nguo, kuuza maji & Ice cream, kuuza genge la nyanya, mkaa, n.k - wenyewe wanasubiri wafunguliwe MIN-MARKET au DUKA LA JUMLA.
Usibweteke, baada ya kuolewa hudumia honey moon yako vizuri kisha rudi kwenye kazi au biashara yako, muombe mumeo akupe muda wa kuendelea na shughuli zako halali au akupe kitu kingine cha kukujenga kimaisha. Maisha ni fumbo, harakati za utafutaji zinaweza kumpeleka mumeo kwenye majanga ya kupata kilema cha mikono, miguu, macho, au kifo.
MWANAUME:👉 Mwanaume bora si yule anayehonga pesa kwa mwanamke wake, bali yule anayemfundisha mwanamke wake namna ya kutengeneza pesa.
MWANAMKE:👉 Mwanamke shupavu hafurahii kuhongwa hela, anafurahia kufundishwa namna ya kutengeneza hela.
By:
RIGHT MARKER - TZ
MHADHARA Na.4
Septemba 18, 2024.