Leo nani anamcheka mwenzake?

Leo nani anamcheka mwenzake?

Fakyuol

Senior Member
Joined
Nov 26, 2023
Posts
148
Reaction score
325
Matokeo yote tayari tumeyapata.

Na mienendo ya timu zetu zote mbili mpaka kufikia hatua hii

Tumeiona!

Simba sc mnyama mkali..kagawana points ugenini

Yanga sc ..wa kimataifa..naye akishabikia sare katika uwanja wa nyumbani

Kishkaji tu eti ni nan anastahili kumcheka mwenzake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yanga anastahili kumcheka Simba sababu mechi ya leo Simba hajaona lango la mwenzie kabisa, bora Yanga karudisha hata hako kamoja, comparisons zingine tuache tu😀
Droo ya 1 - 1 nyumbani? Ingekuwa ni knock out stage Yanga alikuwa ametoka moja kwa moja ilhali Simba angeenda kwenye penati.
 
Tuwapongeze wote. Kwa kweli mchezo wa kandanda umepiga hatua kubwa nchini. Sasa matumaini yapo siku moja Tanzania itakuwemo katika Kombe la Dunia.
Hilo haliwezekani. Wachezaji wazawa sio kipaumbele huko Simba na Yanga.
 
Wote ni pipa na mfuniko. Atayeingia robo fainali ndiyo atamcheka mwenziwe lakini kwa sasa wawe wapole tu
 
Droo ya 1 - 1 nyumbani? Ingekuwa ni knock out stage Yanga alikuwa ametoka moja kwa moja ilhali Simba angeenda kwenye penati.
Hee maajabu haya, timu siku hizi kwenye knock out zinatoka kwa kucheza first leg pekee? Hiyo ni aggregate ya wapi inayochukua matokea ya first leg pekee?
 
Sijui ulijifunzia soka wapi? Ila kwa kifupi; aliyetoa droo ya 0 - 0 ugenini yuko vizuri kuliko aliyetoa droo ya 1 - 1 nyumbani.
Umekariri mpira hujui, Simba alitoa sare ya 0 - 0 dhidi ya UD Songo, unakumbuka second leg ilitokea nini kwa Mkapa? Mpira hauna kanuni, ni kujipanga tu popote unaweza kutolewa.
 
Back
Top Bottom