Raymanu KE
JF-Expert Member
- Jan 20, 2022
- 8,611
- 16,118
Hakuna uhalali wowote ule wa mwanamke kudanga. Hii kitu itachafua maisha yako na itaharibu kabisa maisha yako kiasi kwamba hata ukiwa ndani ya ndoa bado utatamani kudanga.
Kupewa vitu vya bure ni tabia ambayo itakukaa mpaka unakufa, ukizoea vya bure kupewa na mwanaume utaingiwa na tamaa za maisha zaidi, hapo sasa hata utatamani maisha ya juu zaidi, hautaweza kuridhika, na ukifka hatua hiyo kutulia ndani ya ndoa au kuwa na mwanaume wa kawaida kuanza nae maisha kwako itakuwa ngumu.
Unapokuwa na shida kama hivi, omba msaada usaidiwe ila usije fikiria kufanya umalaya, yaani kudanga sababu ya hali ya maisha. Ninakwambia hivi sababu mimi nmeshahuhudia mabinti wengi wadangaji wanapofika 30s maisha yao yanapoanza kujawa na majuto ambayo hawawezi tena kuyerekebisha.
Dada hata maisha yawe magumu vipi usithubutu kudanga.
Muamini Mungu atakufungulia njia na hakika utapata ajira.Usife moyo hayo unayopitia Sasa hivi Ni suala la Muda tu ipo siku Mambo yako yatakaa sawa.
Uzi wa kimkakati huu
Weka Namba tukuchangie mboni hutaki kuweka Namba au umeridhika na hali yako ya kutokwenda kazini au hii ni Chai Bora?Amen [emoji120]
Kwa hiyo hapo kazini unaitafuta laki kwa mwez mzima...?! mishahara wa mwez huu ukiupata embu njoo tandika tafuta mapochi,beg za shule,shuka ingia barabarani ukauze Mambo ya usomi weka pembeni
Weka Namba tukuchangie usitupangeRafiki angu amini unachoamini
Hapa nilipo nina majonzi, roho imeniuma sana kwa kuzaliwa kwenye familia maskini
Ipo hivi mimi kwetu ndio wa mwisho msichana peke yangu kati ya watoto 6.. Mzee wangu alitangulia mbele za haki hivyo tumebaki na mama tu.. hao ndugu zangu wote hawana maisha ya kueleweka isipokuwa mmoja tu angalau yeye ameajiliwa serikalini ndio kidogo anaibeba familia, yeye ameshaoa ana familia yake
Mimi nimeshahitimu chuo nina kama Miaka miwili nyumbani.. nimepata sehemu ya kujishikiza wananilipa 250000.. Kwetu ni bunju nafanyia kazi magomeni kila siku natumia 5000 yaani 3000 nauli 2000 nakula mchana hapo Ndio najibana mno..
Sasa kwasasa Hivi nyumbani Hakuna mtu nipo peke yangu mama ameenda kijijini kwao bibi anaumwa, mama yangu hana kazi ile ya kumtegemea anauza chupa za maji hivyo siwezi kumsumbua kwa chochote, amesafiri hajaniachia hata shilingi 100.. Hakuna chakula ndani Hakuna chochote, nachofanya nikitoka kazini nashukia kwa brother nakuta wamepika nakula naondoka
Leo nimeumia sana sijaenda kazini Nina siku 2 sina nauli hela niliokuwa nayo akiba imeisha nimemuomba bro kasema yeye hana hela hawezi kuwa anatoa hela mara mbili mbili kwa familia yake na kwangu, Kama niliweza kutafuta kazi basi nijitegemee nauli nikitaka kula nije nyumbani,, nikamuuliza sasa nitatoa wapi na Ndio naanza kazi akanijibu nitajua mwenyewe
Hiyo kauli imeniuma yaani anamaana gani kusema nipambane nitafute nauli yaani naitafutia wapi ..
Leo nimeacha kuwa judge Watu na maisha wanayoishi Kama ndugu yangu wa damu ananiambia maneno haya hao wa nnje watanijibu vipi
Ni hayo tu wakuu
Weka Namba tukuchangie mboni hutaki kuweka Namba au umeridhika na hali yako ya kutokwenda kazini au hii ni Chai Bora?
Unawaset watu, huna shida wewe umekuja kupiga story tu mwenye shida hanaga konakona nyingiHapo nimejibana na minyoosho
1.Mama anauza chupa za plastic
2.Unapitia kwa broo kulachakula cha usiku kila siku
3.Nauli imekata kabla ya mwezi kuisha na hujaenda kazini 2days.
Hii story inahuzunisha sana sana.
Pole sana,Mungu akusaidie akupe uvumilivu,natumaini utavuka tuu.Mwanzo mgumu siku zote.
Ila kama umeandika haya kwa ajili ya kuwahadaa watu kwa sababu unazozijua wewe,basi Mungu ataingilia kati
Why wengi wetu wanaamini kuwa nyuzi nyingi ni za kutunga??1.Mama anauza chupa za plastic
2.Unapitia kwa broo kulachakula cha usiku kila siku
3.Nauli imekata kabla ya mwezi kuisha na hujaenda kazini 2days.
Hii story inahuzunisha sana sana.
Pole sana,Mungu akusaidie akupe uvumilivu,natumaini utavuka tuu.Mwanzo mgumu siku zote.
Ila kama umeandika haya kwa ajili ya kuwahadaa watu kwa sababu unazozijua wewe,basi Mungu ataingilia kati
Weka Namba wanaokuletea shida ignore haraka Sisi tutakusaidia km unaona uoga basi acha usiwekeNatamani kufanya hivyo ila kuna watu humu wanaweza kutumia namba yangu kunikejeli
UNASEMA......???Natamani kufanya hivyo ila kuna watu humu wanaweza kutumia namba yangu kunikejeli