Uwesutanzania
JF-Expert Member
- Feb 9, 2019
- 1,380
- 1,686
Ni mimi wako UWESUTANZANIA,.
Katika maisha ya kila siku ya binadamu amekuwa ni mwenye kupitia mambo mbalimbali,.
Yaani kutenda na kutendwa, kusaidiwa na kusaida, kukosea na kukosewa.
Ndipo tumeumbwa na KUSAHAU.
Yaani KUSAHAU kutakufanya uwe huru.
KUSAHAU kutakufanya uwe mtu mpya kila leo na kuendelea na yajayo bila kuteswa na yaliyopita.
Hivyo basi binadamu kamili ni yule mwenye KUSAHAU,.
ingawa wengi mmekuwa wa kumlaumu mwenye KUSAHAU.
mifano:-
-Kuna mtu uliwahi kumsaidia siku moja na alikushukuru sana, ila sasa hivi amekusau kabisa na anafanya mabaya kwako.,
-Kuna watu waliwahi kuwa maadui na kwasasa wamesahu kabisa na ni marafiki .
-kuna watu waliwahi kuwa marafiki wakubwa na kusaidia kwa kila jambo lakini kwasasa hivi ni maadui.
Naam huo ndio ukamilifu wa binadamu.
Binadamu aliye sawa hawezi kuteseka na jambo limepita miaka kumi nyuma au mwaka mmoja nyuma.
Binadamu aliye sawa hawezi kuteseka eti na fadhila za wazazi wake waliomsaidia utotoni,.
Pia hawezi kuteseka na mabaya ya wazazi wake waliomfanyia utotoni.
Binadamu dhaifu tena mwenye mapungufu ndio atakaa kuteseka na fadhila au na maonevu yake miaka nenda rudi.
Binadamu hupaswi kuwa mlipa fadhila siku zote, hata kuhusu uumbaji wa Mungu na fadhila zake hatupaswi kuwa watumwa juu yake. Lazima tusahau ili maisha yaendelee.
Hivyo kama unatenda msaada kwa binadamu yeyote iwe mtoto wako mke wako jirani yako au hata rafiki yako. Msaada wako atausahu tu,
Na pia kama uliwahi mkosea binadamu yeyote basi kuwa huwa huyo binadamu ameshasau mda tu.
Ndio maana hata Mungu mwenyewe kwenye vitabu vyake mnavyoviamini amesema
(Ama kwa hakika binadamu ni mwenye kughafilika na ni mwenye kusahau.)
Na kusahau haijakuja bure umetuumbia ili tuwe huru.
Asante.