Leo ni hukumu ya kina Aveva pale Kisutu, tuwaombee

Leo ni hukumu ya kina Aveva pale Kisutu, tuwaombee

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
Leo tarehe 06 October 2021 ndio siku ya kusomwa hukumu ya kesi inayowakabili aliyekua Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva na wenzake.

Katika kesi hiyo washtakiwa wanadaiwa kula njama, matumizi mabaya ya ofisi, kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu pesa za mauzo ya Emmanuel Okwi.

Mshtakiwa mwingine, Hanspope alifariki hivi karibuni

Wanamichezo hasa soka bila kujali itikadi za Usimba na Uyanga tuungane kuwaombea ili waweze kupata nafuu ya hukumu na ikiwezekana wasikutwe na hatia na waachiwe huru

Michezo ni furaha, michezo ni amani, michezo ni afya japo kua siku hizi ni biashara.
 
Kama Wana makosa kwanini tuwaombee
Wakati mwingine mahakamani ni kama kamari Mkuu. Mtu anaweza akadhani anachomoka kwenye kesi yake mwisho wa siku ikaja kumfunga. Inategemea namna anavyoweza kuziba matobo ya ushahidi dhidi yake na kushawishi mahakama

Ndio maana wengine kwenye rufaa watu baada ya kuhukumiwa na kuadhibiwa huachiwa huru sababu mahakama zilizowatia hatiani mwanzo zilikosea

Tuwaombee tu Mkuu
 
Back
Top Bottom