Blazing Inferno
Member
- May 10, 2021
- 25
- 24
Umeshawahi kukaa chini na kutafakari ni mara ngapi umejikosea kwa kujidanganya kwa kauli “Nitafanya kesho" ! Bila shaka unastahili kujipa adhabu kali ya kutega sikio kwa makini kabisa na kunisikiliza kwa utulivu uliopitiliza maji ya mtungini. “Nitafanya kesho" ni moja kati ya makosa makubwa sana tunayoyafanya tukiwa kama watu wenye malengo makubwa ya mafanikio.
Hapana! Usijidanganye tena kua hauna ndoto yoyote kubwa kwenye maisha yako. Kila mmoja wetu ana ile ndoto kubwa anayotamani kuifikia siku moja iwe anawaza kwa siri ama anashirikisha wengine. Tatizo linakuja pale ambapo tunatumikisha sana bongo zetu kuvuta na kutengeneza taswira ya mafanikio ambayo hatuko tayari kushughulisha mikono yetu ama sehemu nyingine za miili yetu kufanikisha ndoto hizo. Mwisho wake bongo zetu zinajenga tabia ya ku“ fantasize" mafanikio kama vile tamthilia ya runinga ambayo baada ya kuitazama hautoitumia kokote badala yake inakua kumbukumbu isiyo na thamani kubwa kwenye akili yako.
Leo hii wengi wetu tumekua kadi za kumbukumbu (memory cards/ Flash drives) za mipango mikubwa ya mafanikio. Bongo zetu zimejaa mipango mingi ambayo kwa namna moja ama nyingine hatufanyi juhudi za kuhuisha mipango hiyo ibadilike na kua matokeo yenye tija kama tulivyotamani iwe kwenye taswira zetu. Wengi wetu tumepata bahati kubwa ya kutambua vipaji ama vipawa vyetu ikiwemo michezo, sanaa, biashara .... n.k. Pia wako wengine waliobahatika kuhudhuria angalau semina mbili tatu za mafunzo ya ujasiriamali wa aina mbalimbali. Swali ni je? tunasubiri nini kuyafanyia kazi yale ambayo tunayajua tayari?
Tusipotaka kupambana na uvivu wa akili kwa kuziamsha akili zetu zitende yale tunayoyawaza suala la umasikini na kuwatupia lawama ndugu zetu, wazazi wetu, mifumo ya serikali ama wanasiasa halitofika kikomo. Ulimwengu wa sasa haukuhitaji usubiri watu wengine katika mafanikio yako kwasababu kila mmoja anashughulishwa na yake.
Kwa mfano unaweza kukuta kijana ana wazo zuri la mradi linaloweza kumtengenezea kipato kidhi ambacho taratibu kinaweza kubadili maisha yake lakini bado kijana huyu akaogopa kutekeleza anachokiwaza. Akahofia hasara ya kuanzisha mradi kwa kianzio ama mtaji mdogo usiyo na uhakika wa faida bila ya kuwaza hasara anayoipata kwa kupoteza muda akiisubiri pesa kubwa ya mtaji ama mazingira mazuri ya kianzio ambayo ni ya kufikirika.
Watu wengi tumekua tukighailisha utekelezaji wa mipango yetu muhimu kwa kusubiri mitaji mikubwa ambayo kiuhalisia kamwe haitokuja kutunguangukia miguuni kwetu kama majani ya miti ama kutunyeshea kama mvua. Tuna ile hali “siwezi kuanza na mtaji wa shilingi laki moja nasubiri milioni mbili acha hii niifanyie mambo mengine..." Swali ni je! Umeagana na nani atakaekupa hiyo milioni mbili na ni lini? Hatimaye kijana anapoteza miaka akisubiri milioni mbili itayokuja kwa mkupuo huku akiendelea kutumia zile elfu hamsini hamsini akivuta muda!
Tukumbuke kua ata hii ‘leo’ ilikuwa ni ‘kesho’ ya jana, ‘kesho kutwa’ ya juzi, ‘wiki ijayo’ ya wiki iliyopita, ‘mwakani’ ya mwaka jana. Siku za mabadiliko binafsi ya kiuchumi hazisubiri siku yenye jina fulani bali zinaamuliwa na utayari wetu wa kuchukua hatua kuyaelekea mafanikio. Ni kweli kwamba kila biashara ina kupata faida na hasara lakini hilo halitupi udhuru wa kuogopa kufanya ama kujaribu. Kujaribu na kufeli na kujaribu tena kwa mara nyingine ni alama tosha kua tumedhamiria kufanya mabadiliko. Kuogopa kujaribu ni kuulea umasikini kwa mapenzi mazito.
Huwezi kupiga vita na ushinde bila kupata japo jeraha dogo. Kufeli pamoja na kupata hasara ni Sehemu ya majereha madogo katika vita kubwa vya utafutaji ambayo baada ya mafanikio utakua ni
sehemu ndogo ya historia ya mapambano yako dhidi ya adui umasikini.
Chukua pesa wekeza kwenye biashara unayoona itafaa, ikileta hasara jifunze ulipokosea, tafuta pesa tena weka kwenye biashara ukipata hasara jifunze tena kisha fanya tena ukiwa na ari ileile. Fanya hivyo mpaka siku ambayo utakua mkomavu kibiashara ama katika chochote unachofanya na hasara itakapogeuka kua ndoto inayokuogopa.
Pia nipende kukumbusha kua tunapoyafikiria mafanikio hatutakiwi kujifananisha na baadhi ya watu waliopiga hatua kubwa tayari kama Mo Dewj ama Bakhressa kwasababu hatuwezi kuwafikia kirahisi hivyo inaweza kututoa hamasa ya kujaribu japo si vibaya kuwatumia kama viigizo.
Kwenye suala la utafutaji juhudi zipe asimilia 90% bahati ipe 10% kwasababu idadi kubwa ya waliofanikiwa waliweka juhudi sana kulinganisha waliofanikiwa kwa kubahatisha ambao ni wachache sana (mfano Laiza wa Tanzanite)
Kila mmoja ana uwezo wa kua na ndoto lakini si kila mmoja ana uwezo wa kuziishi ndoto zake, kinachotafautisha wanaoishi ndoto zao na wanaoshindwa ni juhudi na kujitambua. Ukijitambua wewe ni nani na unataka nini, kwa kiasi gani na ndani ya muda gani basi hautojiingiza kwenye kundi la ulevi wa kinywaji “nitafanya kesho ” ni kinywaji kibaya sana na hakijawahi kumuacha salama yoyote aliyewahi kukitumia.
Waswahili tuna msemo “hakuna anaeijua kesho" sasa kama tunakubaliana hivyo inakuwaje tuahidi kuanza kufanya mambo katika muda ambao hatuujui (kesho) badala ya kufanya leo ambayo tunaijua. Napenda nieleweke kwamba kesho ninayomaanisha hapa ni ile tabia ya kughailisha mambo na kusema nitafanya wakati fulani ujao angali uko uwezekano mkubwa ukayafanya mambo hayo ndani ya kipindi hicho na si kesho ya kuzama na kuchomoza kwa jua ya masaa ishirini na manne.
Hapa ndani pia JF naamini wako watu wengi wenye uwezo mzuri wa kuandika makala nzuri zenye tija wakaweka hapa Stories of change lakini yawezekana kila siku wanajiahidi kwamba wataandika kesho ambayo haijawahi kufika. Kesho si muda wa kuanza kufanya unachoweza kufanya, kesho ni wakati wa kupata matokeo ya unachoweza kufanya leo. Kesho si wakati wa kupanga mihangaiko, kesho ni wakati wa kusherehekea mihangaiko ya leo.
Kesho ni adui mlaghai wa maendeleo, kesho ni dubwana linalojiandaa kukucheka kwa kuichezea leo yako, kesho ni uraibu (addiction) utaokufanya utake kesho nyingine. Kumbuka leo ni kesho ya jana na kesho ni aidha majuto ama mafanikio ya leo. Uamuzi uko kwenye mikono yetu tunataka kesho iwe nini kwetu aidha siku ya matunda ama siku ya majuto.

Upvote
2