Leo ni kilele cha wiki ya tafsiri

Leo ni kilele cha wiki ya tafsiri

Joined
Apr 18, 2018
Posts
5
Reaction score
4
Tujue kwanza tafsiri ni nini?

Tafsiri ni uhawilishaji wa maudhui kutoka lugha moja kwenda nyingine. Tafsiri inakupa maana iliyolengwa katika lugha ya kwanza kwenda lugha lengwa.

Kuanzia tarehe 24 septemba ni wiki ya tafsiri ambayo kilele chake ni 30. Kwa nini tarehe 30? Ni kwa sababu ilikuwa ni namna ya kuanza kumuenzi mtafsiri wa kwanza aliyejulikana kwa jina la Saint Jerome ambayo hiyo ilikuwa tarehe yake ya kifo chake.

Hii iliibuka kutokana matokeo ya kuendelea kukua kwa mitagusano miongoni mwa jamii mbalimbali. Kwa hiyo ili jamii ipate mawasilano hayo ilibidi iwepo tafsiri ya kuwapa taarifa wale ambao hawakuelewa lugha zile.

Ni nani mfasiri?
Moja awe mjuzi na mahiri wa lugha chanzi (ya kwanza) na lengwa (lugha ya pili) inayofanyiwa tafsiri.
-Ajue utamaduni wa lugha anazozifanyia kazi.
- Awe na kaida ya kusoma ili aweze kukabiliana na dhana mpya zinazoibuka.

Kwanini ilikuwepo taaluma ya tafsiri?
Mwanzo kulikuwa na watafsiri huru na horela matokeo yake tafsiri zilikuwa tenge zisizokuwa na ulinganifu wa maudhui kwa jamii ya pili. Hiyo ikawa sababu ya kuona umuhimu wa taaluma ya tafsiri. Kwa sasa tafsiri inafundishwa kwenye vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini.

Nafasi ya tafsiri katika jamii ni kuwezesha maarifa yaliyo katika jamii moja na kwenda katika jamii nyingine.
Kwa sasa ipo miradi, vitabu na makala hutafsiriwa kutoka lugha moja kwenda nyingine. Wawekezaji wanapata nafuu kupitia huduma ya kutafsiri miradi pale inapohitajika kufanyiwa hivyo.

Karibu katika ulimwengu wa tafsiri.
 
Back
Top Bottom