Uzi wa 2019, siyo mbaya.
Marehemu Edward Moringe Sokoine alikuwa mtu maarufu.
Jasiri, aliyethubutu.
Nikikumbuka ni kama aliwahi kuwa waziri kisha akaenda kusoma huko ughaibuni.
Alipoteuliwa kuwa waziri mkuu ni kama mteuzi wake alishtukia uwezo wa utendaji wake
Ikafika siku ya kufunga kikao cha bunge huko dodoma.
Wakati huo tukiona bunge laivu.
Aliaga kuwa tutaonana bunge lijalo. Hakujua masikini nini kitamfuata.
Ile anarudi zake dsm kwa njia ya barabara katikati ya pori ndipo alipokutana na gari landcruiser mkonga nje ikiendeshwa na dogo mkimbizi ikamvaa uso kwa uso.
Masikini Moringe Edward, safari ya maisha yake ikaishia pale.
Alizikwa kwao, japo miaka kadhaa nilisikia wanataka kuhamisha mwili maana boma limehama. Sijui kama zoezi lilifanikiwa.
Tuliomfahamu Edward Moringe Sokoine tunamkumbuka.
Lala salama huko uliko shujaa wetu, je umewahi kukutana na Mwalimu Nyerere huko, msalimie.