Leo ni kumbukumbu ya Justine Kalikawe ,je ni unamkumbuka kwa lipi zuri?

Leo ni kumbukumbu ya Justine Kalikawe ,je ni unamkumbuka kwa lipi zuri?

Namkumbuka Justine Kalikawe dah!! Alikua anajua Sana kuimba!
 
Namkumbuka kwa nyimbo zake,kuna nyimbo yake moja nilikuwaga

nausikiliza sana
 
"Ningekuwa na mabawa ningeruka kama ndege, lakini mimi mwanadamu.."
jamaa alikuwa vizuri, angekuwepo angeupeleka mziki wa rege kwenye leval nyingine.
alale pema peponi
 
wanasema hatuwezi kupiga hatua
kuthaminiwa wala kutambuliwa
eti sababu sisi watu weusi tumepewa laana
usiseme hivyo ebu acha kufuru aliye tuumba Apendezewi hivyo

Mwl Nyerere, Kwame Nkurumah,
mizimu yao ilitokea Wapi?
 
Huyu jamaa nilikuwa nafahamu nyimbo zake.. But mwenyewe sikumfahamu.. Nashukuru kwa picha mkuu
 
kuna nyimbo yake moja ilikua ikiimba..wewe mama wa kambo usiwe sijui nn....nilikua nikiiweka kanda yake,mama niliyekua naishi nae lazima aitoe ile kanda,and finally aliitupa ile kanda......RIP kamanda
 
Wimbo wa Mv Bukoba,(Nanukuu kidogo,husikitumie cheo chako kama dhamana ya matakwa yako utasababisha ajali kama ya mv bukoba
 
....classmate muhimbili primary school, a friend and a neighbour Upanga.

Miaka mingi imepita, kumbukumbu zimebaki sie tukiwa kijiweni Boy Scout, twamsikiza Justin Don Bosco akifanya Rehearsals.

Rest in Peace bro.
 
kuna nyimbo yake moja ilikua ikiimba..wewe mama wa kambo usiwe sijui nn....nilikua nikiiweka kanda yake,mama niliyekua naishi nae lazima aitoe ile kanda,and finally aliitupa ile kanda......RIP kamanda

ukiwa mama wakambo, usiwe kaa la moto, utaunguza nyumba watoto wakose kuishi na baba yao,
ona hizi familia zinavyo vurugika, zinaangamia watoto wanalanda landa mitaani......
He was a legend
 
"Mbona unanifuatafuata na maneno eti Jastin Kalikawe hawezi ragga, mawazo yake yote yapo kwenye reggae, ngoja nikufahamishe kwanini ni mtu wa reggae, ukipiga reggae ndani yake kuna ragga, ukipiga ragga ndani yake kuna reggae"
 
ni kalikawe pekee aliyeweza kuimba reggae za kiswahili zikapendeza. miaka ya 2005 au 2006 kuna jamaa anaitwa half cast alipiga reggae mbili tatu za kiswahili alijitahidi sana sijui amepotelea wapi
 
ukiwa mama wakambo, usiwe kaa la moto, utaunguza nyumba watoto wakose kuishi na baba yao,
ona hizi familia zinavyo vurugika, zinaangamia watoto wanalanda landa mitaani......
He was a legend
sijui yule mke wake mzungu wahaya washamuacha?
 
Back
Top Bottom