Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,053
- 6,304
Na Joseph ShaluwaFAINALI za kumsaka supastaa wa Bongo katika Shindano la EBSS zinafanyika leo Ijumaa, Novemba 9, mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar huku mshindi akiwa siyo siri, Ijumaa linakuhabarisha.
Watakaomenyana jukwaani ni Walter Chilambo, Salma Abushir, Nsami Nkwabi, Nshoma Nghangasamala na Wababa Mtuka (pichani juu).
SIRI NI HII
Piga ua, washiriki Walter Chilambo, Wababa Mtuka na Salma Abushir ndiyo watakaoingia 3 Bora na mmoja wao ataibuka mshindi atakayekomba Tsh. 50 milioni.
Washiriki hao wanapewa nafasi kubwa kutokana na sababu tofauti ikiwemo vipaji halisi, kutawala jukwaa na uwezo wa kutumia ala mbalimbali za muziki.
WABABA
Tangu mwanzo wa shindano ameonekana kuwakonga watazamaji vilivyo, ukiachana na sauti, kitu cha kipekee alichonacho ni kutawala jukwaa, sifa ambayo inamfanya awaache wenzake mbali na kumpa nafasi ya kushangiliwa kila anapopanda jukwaani.
Pamoja na uwezo wake, huenda Wababa akaambulia nafasi ya pili, kama majaji watazingatia kigezo cha kupishanisha jinsia za washindi katika mashindano yao.
Mwaka jana alishinda Hajj Ramadhan, Mariam Mohammed mwaka 2010, Pascal Cassian mwaka 2009, Misoji Nkwabi mwaka 2008 na aliyefungua dimba alikuwa ni Jumanne Idd mwaka 2007.
SALMA
Ni binti mdogo lakini mwenye uwezo mkubwa wa kucheza na sauti na kutawala jukwaa lakini sifa kubwa waliyokosa wenzake ni namna anavyochezea nyuzi za gitaa; sifa hii ndiyo inayomfanya aitwe mwanamuziki.
WALTER
Sifa kuu kuliko zote kwa Walter ni namna anavyoweza kuimba nyimbo za aina zote kwa ustadi mkubwa na sauti inayoweza kupanda na kushuka kulingana na wimbo aliouchagua.


