Leo nilipokuwa namsikiliza Mdude imenijia kwenye akili, huyu jamaa kuna analolitafuta na naamini atalipata

Leo nilipokuwa namsikiliza Mdude imenijia kwenye akili, huyu jamaa kuna analolitafuta na naamini atalipata

Kaselele

Senior Member
Joined
May 19, 2022
Posts
171
Reaction score
476
Muda mwingine huwa najiuliza huyu Mdude anapata wapi kiburi cha kuitukana serikali tena hadharani?

Hivi kweli mtu hawezi kuwa mwanaharakati bila kutukana viongozi wa serikali, kuna ulazima gani kwa mwanaharakati kutumia matusi na kuhatarisha usalama wa taifa?

Anasema ataitisha maandmano kama ya Kenya, amesahu kujiuliza maandamano ya Kenya yameishia wapi?

Je, bei za bidhaa zimeshuka kupitia maandamano yale? Je, mswaada wa fedha haukupitishwa?

Binafsi sioni hawa wanaharakati wa aina ya Mdude wapo kwa maslahi mapana ya Taifa.

Si kitu kizuri kutumia uanaharakati kwa maslahi ya mtu binafsi.

Mdude haya anayoyafanya ni kwa maslahi ya nani?
 
Hakuna mtu mwenye akili timamu atatilia maanani maneno ya mvuta bangi na mbumbumbu

Slaa ana hasira ya kuvuliwa Ubalozi ndio maana anatukana.

Mwabukusu Toni ya sauti na maelezo amepunguza kidogo msimamo ndio maana unaona anataka mazungimzo.
 
Mdude amekosa lugha nzuri ya staha.

Ukiachana na udhaifu wake kwenye jambo hilo hoja zake kuu kuhusu IGA inayo husu bandari na DP World ni za msingi sana na za faida kwa watanzania wote.

Bila kusahau hoja ya Katiba mpya nayo ni ya msingi ingawa naona tatizo la Tanzania siyo katiba au sheria maana hata Katiba na sheria za sasa vinavunjwa na viongozi na mafisadi bila kuwajibishwa. Tatizo kubwa ukosefu wa maadili, tabia zetu n.k.
 
Licha ya hoja na madai ya msingi ya wanaharakati/wapinzani wanayotoa dhidi ya serikali ila swala la lugha za staha ndio kitu ama mahala wanapofeli, hili Mboye alishazungumza alipotoka kufanya kikao na rais SSH ila ni kama viongozi wao hili somo walishafeli yanaingilia huku na kutokea kule.
 
Wewe unaandika hayo kwa maslahi ya nani!?
 
Back
Top Bottom