Leo nimeiweka line ya TTCL pembeni, Nyumbani kuchungu

Leo nimeiweka line ya TTCL pembeni, Nyumbani kuchungu

Tunzo

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
4,082
Reaction score
2,402
Kweli nyumbani kulianza kunoga, basi kadhaa tukarudi kwa machale, kukawa na ile huduma ua BUFEE (MPYA) ya kujipangie, yani kama nataka MB tu najichagulia na kama ni dakika tu, nachagua, na kama ni vyote najipangia kua MB ngapi, Dakika ngapi na sms ngapi, najiunga ninavyotaka.

Ila naona siku kadhaa wamepandisha bei za kujiunga ambavyo ni zaidi ya mitandao mingine. Ni bora 1000 ujiunge mitandao mingine kuliko Bufee ya TTCL, yani pamoja na huduma za kawaida sana mmeamua kupandisha vifurushi.

Mfano mitandao mingine 1000 unapata MB 500, dakika 40 na sms 10, ukija TTCL ili upate hii lazima uwe na karibia 1200, bado mwendo wa kawaida, Bora niiweke pembeni.

Kwaherini, mkijirekebisha nitarejea
 
Mtandao wa serikali ndiyo unakuwa na vifurushi vya bei ghari kuliko mitandao ya simu ya makampuni binafsi.
Kuna mjinga mmoja atakuja kukuambua watanzania tuwe wazalendo. Kwa hali hii HAPANA
Sijajua wanawaza nini
 
Mimi ndio nautumia ni bei Chee kuliko mitandao mengine sema hamuujulii ofa zake


Hivi unajua kifurushi cha bufee wewe?
 
Shida ya huu mtandao uko sehemu kubwa mjini ukienda vijijin haupo ata ukitoka kidogo nje ya mji hamna network ni shida halotel wakiboresha huduma zao watapata wateja wengi na wameenea Kila Kona mjini wapo vijijin wapo
 
Mimi ndio nautumia ni bei Chee kuliko mitandao mengine sema hamuujulii ofa zake


Hivi unajua kifurushi cha bufee wewe?
Tena hapa ndio wamechemka kwa kupandisha, mimi natumia hicho cha bufee, wanakudangaja,. Jiunge MB 500 dakika 40 na sms unazopata kwa tigo 1000 kama hiko haizidi
 
Back
Top Bottom