#COVID19 Leo nimekwenda Muhimbili kuchanja Corona halafu nimeogopa, nimerudi

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,095
Reaction score
4,632
Leo, yaani jana Jumamosi nimekwenda Muhimbili kuchanja Corona. Nimeingia katika geti, nilikuwa nashangaa shangaa pale akaja mwanamke mmoja akaniuliza, "Kwani ulikuwa unataka kwenda wapi?" Nikamwambia nataka kuchanja Corona. Akaniambia pita pale hospitali ya Jakaya, halafu mbele kule kuna jengo la kutibu watoto, ndipo wanapochanja Corona.

Kwa hiyo nikaenda mpaka kule, lakini nilipofika pale nikaogopa kuingia ndani, nikarudi. Nikaamua kwamba labda naweza kufanya mazoezi ya yoga, laya yoga, raja yoga, sahaja yoga, whatever, lakini sitaki kuchanja.

 
Heri yako; kwani ulizaliwa lini? Watu wote waliozaliwa Tanzania kuanzia mwaka 1970 huwa wanachanjwa BCG dhidi ya kifua kikuu; je uliiogopa BCG pia ukarudi nyumbani?
 
Kwani ulipotoka nyumbani ulikuwa bado hujafanya uamzi wa kwenda kupata chanjo?

Fanya hivi, mchukue mama watoto akushike mkono na kukuongoza hadi hapo wanapotoa chanjo. Ahakikishe amakukalisha juu ya kiti na kutoa maagizo maalum kwa mtoa chanjo asiruhusu utke hapo tena bila chanjo kukamilika.
 
Heri yako; kwani ulizaliwa lini? Watu wote waliozaliwa Tanzania kuanzia mwaka 1970 huwa wanachanjwa BCG dhidi ya kifua kikuu; je uliiogopa BCG pia ukarudi nyumbani?
Hao wanachanjwa wakiwa watu wazima au watoto wasiojua hata kukataa?

Na kama za muhumu Kwa Nini zisisubili mpaka MTU awe mtu mzima ajue kukubali au kukataa.
 
Wewe msanii mtoto, yaani huyo mwanamke kakufuata wewe na kukuuliza! Alikaa getini kwa ajili yako tu! Hadithi za kitoto hizo.
 
Unaogopa bure tu. Mimi nimechanja na niko vizuri tu.

Nilipata kihoma fulani tu, nikanywa maji na kumeza Panadol basi.
Niliweza kuchanja kituo cha afya yombo vituka kwa kweli muamko ni wa chini sana ila baada ya kuchoma hali yangu ilikuwa kama homa nikapata panadol lakini naendelea vizuri ila ya waziri gwajima sijajaribi
 
Wewe hujaenda muhimbili, sababu hapo wanapochanjia, sio jengo ni jukwaa la hema.
 
Hicho kitabu cha Laya Yoga nimekisoma and it proved to be quite interesting.



 
Kachanje pls, virus ni vibaya sana.
 
Miezi kadhaa iliyopita watu karibia 5000 walikuwa wanakufa kwa siku.
sikatai, lakini bado ukweli unabakia kuwa ni kweli kabisa hakuna aliyewahi kuona kirusi. Wataalamu wengi wanasema hivi: Uwezekano mkubwa ni kuwa watu wanadhurika kutokana na sumu, kitu wanachoita toxemia. Najua ni vigumu SANA kuwashawishi watu kuhusu mambo ambayo wameaminishwa kwa miaka na miaka, lakini waandishi wa kitabu kiitwacho VIRUS MANIA wanasema hivi LOLA70


Tukitaka kujua uongo ambao dunia imejazwa sana, ni lazima tuwe tayari kuwa na mtazamo TOFAUTI kabisa.
Lakini tukiwa RIGID, tutadanganywa hadi tunaingia kaburini.

Tunapokutana na misimamo tofauti, ni muhimu tujiulize, HIVI INAWEZEKANA EE? Kisha unaanza kufuatilia. Utakutana na mambo ya ajabu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…