Leo nimemkumbuka mwanamuziki Kikumbi Mwanza Mpango, King Kikii, aliposema "Tushike ya kwetu, tusiwape muda karagosi", karagosi ni nani?

Leo nimemkumbuka mwanamuziki Kikumbi Mwanza Mpango, King Kikii, aliposema "Tushike ya kwetu, tusiwape muda karagosi", karagosi ni nani?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
leo nikiwa natoka mahali kwa kutumia public transport, ukapigwa wimbo wa King Kikii, kitambaa cheupe, hivyo from no where, nimetokea kumkumbuka mwanamuziki mkongwe huyu, jina kamili ni Kikumbi Mwanza Mpango, aka King Kikii, kumbe pia alikuwa na vibwagizo fulani vya kisiasa vya kiaina.

Kwenye wimbo huo, kuna versi aliimba
"Bongo ina mambo mengi mama eeh
Kila kukuchapo kuna mambo mapya,
Tuyazingatie ya kwetu,
Wala tusiwape muda Karagosi".

Karibu msikilize


Verse hiyo imenifikirisha sana, haswa kwenye muktadha wa uchaguzi mkuu wetu kwa upande wa urais.

Japo kikaragosi kwa kizungu ni cartoon, caricature, marionette, jee hapa kwenye neno Karagosi, King Kikii alimaanisha nini?.
Nani ni Karagosi au karagosi ni nani?.

Sijui kwa sasa King Kikii yuko wapi na ana hali gani, hivi kumbukumbu kama hizi, hazichelewi kumuibua na wote tuksmfahamu Karagosi ni nani!.

Paskali
 
Mtunzi wa wimbo huo wala hakua na maana unayoitaka mkuu.

Na kama una lengo la kumbeza au kumtweza au kumkejeli mgombea fulani, basi unapoteza muda wako.

Kila mtu kwa nafasi yake anatambua anataka nini katika uchuguzi huu, kwa jasho na damu, kura zitakwenda kuamua hatma ya nchi kwa mara ya kwanza. Kinyume na hapo ..............
 
P waache watu watumie haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi wanaowaona watawaletea maendeleo

Wewe ni mwandishi nguli. Ingebidi ujikite zaidi kuhamasisha watu walojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura wajitokeze tarehe husika. Ila hii ya kupigia chapuo ule upande wako unatufikirisha sana jirani
 
Wanabodi,
leo nikiwa natoka mahali kwa kutumia public transport, ukapigwa wimbo wa King Kikii, kitambaa cheupe, hivyo from no where, nimetokea kumkumbuka mwanamuziki mkongwe huyu, jina kamili ni Kikumbi Mwanza Mpango, aka King Kikii, kumbe pia alikuwa na vibwagizo fulani vya kisiasa vya kiaina.

Kwenye wimbo huo, kuna versi aliimba
"Bongo ina mambo mengi mama eeh
Kila kukuchapo kuna mambo mapya,
Tuyazingatie ya kwetu,
Wala tusiwape muda Karagosi".

Karibu msikilize


Verse hiyo imenifikirisha sana, haswa kwenye muktadha wa uchaguzi mkuu wetu kwa upande wa urais.

Hapa kwenye neno Karagosi, King Kikii alimaanisha nini?.
Nani ni Karagosi au karagosi ni nani?.

Paskali

Msituchanganye na nyie sisi tunataka Lissu ili paskali urudi kwenye ile ofisi ambayo pango lake ni mshahara wa DC
 
Karagosi ni huyu bwana aliyetoka ng'ambo na katika huu uchaguzi anajiona kama Simba kumbe ni paka aliyechangamka....anaamuru barabara zifungwe huyu kweli ndio ataleta maridhiano huyu,anawatukana polisi hana adabu anaropoka tuu.

Huyo ndio Karagosi anayemsema Mzee wa kitambaa cheupe na HAKIKA TUSIMPE MUDA KWELI KWELI.

October 28th kura za ndio ni kwa JPM

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Angekuwa Mtanzania mwenzetu angeweza kutumia Mabeberu kina robert kuharibu amani ya Nchi yetu ?
Beberu yoyote hawezi kuharibu amani ya nchi yetu, amani tuiharibu wenyewe halafu tumsingizie beberu.
P
 
Pascal kachukue buku7 yako upite hivii...maisha yanaenda kasi sana

si baadae unakuja kulialia hapa ohhh sijapewa mgao nimepunjwa...chukua chako mapema hata huo udisii utausikia

unadhani kikaragosi ni nani kama siye weye? usikilize vyema.King Kiki amekutungia ww hapo Mayala
 
Back
Top Bottom