Leo nimeona mwenyewe usumbufu wa polisi wa usalama barabarani dhidi ya magari ya mizigo

Kiongozi una gari, inavyoonyesha huna, siku umenunua tena iwe yenye 0 km, ndipo utajua ukubwa wa tatizo lilivyo, uspotoa anakukatia risiti ya faini ili kukukomoa, hii tatizo ni kwa kila geti walilosimama tena ni nchi nzima
 
Kirikuu, Canter na TownAce wanaziita "walinyama" kwakua wakikupiga tu mkono hawana kusumbuana ni buku au buku mbili
 
Toa pesa ya kubrashia viatu, wakikupiga vyeti utakuja ulalialia humu
 
Leta ushahidi wa picha mnato au video
 
Kwa kuwa mamlaka zote zinaelewa kinachoendelea, nadhani bora wangeweka kiwango cha kulipa kwa siku kuwa ni halali, na unapolipa upewe utambulisho wa siku hiyo ili kuonyesha kwenye vituo vingine.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 

Wanakagua magari tu? Si wakague na mabarabara, vipuri, mafuta, mafundi hadi polisi kabisa.

Barabara vimeo, vipuri vimeo, mafundi vimeo, mafuta vimeo, polisi vimeo nk magari yanakuwaje imara?

Si kuwaonea wenye magari tu?
 
Mkuu alishasema hapo ndo wanapopatia ela ya kununua hata dawa za kubrush viatu
 
Sasa mbona hamna sehem uliyoombwa rushwa kwenye maelezo yako? Kama kaomba lesen mpe lesen alaf kauka anahaki ya kukagua ila hana haki ya kuomba rushwa.

Kwahiyo hapo kosa ni la Dereva wako alietoa rushwa bila kuombwa
Huenda unaishi shamba au ni askari traffic
 
Wew jamaa acha kupotosha watu,
Ina maan kila mwenye gari alishawah kutoa rushwa kwa Traffic?
Kosa utakalolifany hata kama gari ni 0 km ndo litakalokuhukumu,na wew kulingana na kwamba hukujiandaa kwa hukumu hiyo unajikuta unatoa hiyo unayoiita Rushwa ili tu usihukumiwe,
Kiongozi una gari, inavyoonyesha huna, siku umenunua tena iwe yenye 0 km, ndipo utajua ukubwa wa tatizo lilivyo, uspotoa anakukatia risiti ya faini ili kukukomoa, hii tatizo ni kwa kila geti walilosimama tena ni nchi nzima
 
Kuna taasisi ilizindua kimfumo fulani ati cha kukamatia wala rushwa, najifunza kuwa ilikuwa mfumo wa ulaji hauna tofauti na ule wa SIM card moja mitandao yote na hata lile dudu liliitwa BRN, yote ni janjajanja ya kula pesa ya umma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…