Leo nimerudia kuzisikiliza Msinitenge, Ni Kazeze, Kosa la Marehemu, Bush Party na Homa Dunia

K sal ni mkenya? Usije ukawa unachanganya na K South ambaye ni marehemu.
 
Mwenye hizo ngoma zote zilizotajwa hapo juu atuwekee hapa tukumbike ujana wetu.
 
Yeah…
Yeah…
Hakuna S bila O
L bila O
Mwingine aitwe’ Thang bila Solo
Shupavu’ awajibike kama Apollo
Jay, Afande!
Ni ukuta’ wapi uchochoro?
Hakuna S bila O
L bila O
Mwingine aitwe’ Thang bila Solo
Shupavu’ awajibike kama Apollo
Jay, Afande!
Ni ukuta’ wapi uchochoro?
Yo Naghani’ ni mtazamo wa fani
Ile dhana ni uhuni wameleta hawa katuni
Kuna ku-rap na kumbwata
Ma-reaper na ma-rapper
Katuni, Tungo tata
Wapi ulipo we jaku?
Unakuwa mtumwa ili upewe promo kuuza
Au kama ni binti’ ukalale kwa prodyuza
Ma-Promoter wana uma tu’ hawajui na kupuliza
Na siku wakipuliza jua kidonda kishaoza
Natamani kuwa huru mnyonyaji asinidhuru
Wanaitwa “ma-Emcee” hawajui mitindo huru
Huu mtazamo wangu’ naona vingi vioja
Yaani watangazaji sasa’ ndo ma meneja
Vidato sita nlivyopitia
Ndivyo vinavyonisaidia
Mbunifu ukiizingatia
Hata wakinibania
Ni kipaji tu
Ni mtazamo tu
Msikasirike wash’kaji
Haya mawazo tu
Ulamaa…
 
Solo Thang alifunika wote hapo
 
Ushawahi sikiliza ngoma ya Boss kaimba Ferooz ft Solo Thang &Juma Kiroboto Nature???
Kama unaangalia movie vile
 
Machozi yanatoka ishara homa ya dunia
Binadamu wanyama ndege wote mbona mnalia
Parapanda italia
Mito milima mabonde vyote vitaangamia
Madaktari waganga ujuzi washautumia
Wamemzunguuka mgonjwa homa ya dunia
Waumini wamemsalia
Na bado mikononi akawafia...
 
Kwenye Party/Party by KR MULLA nadhani hii nyimbo ilikuwa ndio foundation ya mziki wa sasa. Mdundo wa hii nyimbo iliuwahi muda.
 
Ukipima hiyo mistari na uzito wake hakika solo ni mnyama sana!
 
Naomba kuuliza kwa wataalam wa muziki. Hivi singeli Ina vina na mizani?? Au huyu muimba singeli akiwa studio neno linalomjia kichwani ndio anatamka tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…