Leo nimetembelewa na TBC ili tufanye kipindi kuhusu Mzee Abeid Amani Karume

Leo nimetembelewa na TBC ili tufanye kipindi kuhusu Mzee Abeid Amani Karume

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KARUME DAY NA TBC

Leo nimetembelewa na TBC ili tufanye kipindi kuhusu Mzee Abeid Amani Karume.

Mtangazaji Bakari Msuya kaniuliza maswali mengi.

Nimemweleza Mzee Karume nikianza na uhusiano wake na watu wa Dar es Salaam katika miaka ya 1940s hasa na viongozi wa Young Africans Football Club.

Nimemweleza Mzee Karume akiwa na viongozi wa TAA yeye akiwa kiongozi wa juu katika African Association uhusiano ambao ulimsaidia Karume kuunda Afro Shirazi Party (ASP) mwaka wa 1957 kwa msaada mkubwa wa Nyerere na TANU.

Tukaja katika Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano mwaka wa 1964.
Mwalimu Nyerere na viongozi wengine wa TANU hawakuwa mbali na matukio yote haya ya kihistoria.

Kipindi hiki kitarushwa leo baina ya saa moja na saa tatu usiku.





 
Hivi ni wapi kuna hifadhi ya historia za Tanganyika na Zanzibar katika maandishi?
 
Nimekufuatilia mzee upo vizuri na agizo lako la kututaka tusome kitabu Cha kwaheri ukoloni, kwaheri Uhuru nitalizingatia.
 
shekh mohamed said hii ni tunu ya taifa inabid wanahistoria mkae nae ili muandike historia ilio sawa ya nchi yetu
 
Back
Top Bottom