Leo nimevikumbuka vifinyo vya mama jamani

Chakorii

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
18,773
Reaction score
51,429
😅😅😅nimejikuta nacheka kifala sana. Aki tena.

Nakumbuka kuna siku nilimuomba mama hela ya daftari enzi hizooo😅😅niko darasa la tatu akaniambia nitakupa pesa ya daftari kesho nenda shule hivyo hivyo😔😔 nikamtegea katoka nje hapo niko na ufagio wangu na kidumu cha maji🤪🤪 si nikamuibia hela bhna nikaenda kununua daftari😆😆 mbona shughuli niliipata mimi jamani😂😂

Yule mwanamke anajua kufinya jaman kha🤣🤣 nilifinywa mimi..😄😄😄mpka nikahisi kutapika damu..halafu alikuwa ananifinya huku anacheka unaweza kujua unang’atwa na siafu😅😅

Nakumbuka aliniambia ninakupa kipondo kwa sababu umeiba na sio kwa sababu umenunua daftari.

Ama kweli mtoto usimnyime adhabu.😅😂vile vifinyo vilinirudisha kwenye mstari wallah.😂😂

Sijui hata imekuwaje leo kukumbuka mapigo konki ya mama Chakorii😂😂😂
🥂🥂🥂🥂🥂🥂🥂🥂🥂🥂🥂🥂
 
[emoji3591][emoji3591][emoji3591]Wazazi wetu waliyajua majukumu yao na tuko hivi tulivyo sababu walitulea vyema. Tungelelewa kama hawa mabroila wa kisasa wanavyolelewa sidhani kama tungekuwa hivi tulivyo. Mungu Awabariki wazazi wetu na kuwapa maisha marefu [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Na wale waliomaliza safari Mungu awarehemu huko walipo.
 

Amen mkuu.
Ni kweli kabisa wazazi wetu walijua nafasi zao na majukumu ya ulezi waliyasimamia vizuri.

Enzi hizo utandawazi ulikuwa haujashika hatamu😅😅
Siku hizi hata na mfumo wa maisha umebadilika pia mkuu.

ILa nilikuwa nachezea kipondo jamani kha🤣🤣
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaani nakumbuka kuna siku kidogo nilale nje kisa nimekimbia adhabu nachungulia tu mama katoka jikoni kaingia sebuleni hana muda giza nalo hilo hadi wanakaribia kulala mfanyakazi wa mifugo kazunguka zunguka kaniita njaa imenishika[emoji38][emoji38] kaniita jikoni ugali umebakizwa sasa mama sijui alimwambia kamsake aje aleee au vipi [emoji23][emoji23] but mama respect kwake
 
Natumaini yu mzima wa afya akikuangalia binti yake ulivyo katika mstari sahihi.

Yes mkuu yu mzima kabisa na namshukuru Mungu kwa ajili yake.Baba Mungu aendelee kumtunza.

Namkumbushiaga nikiwa nae namwambia “shoga angu na wewe ulikuwa unanifinya utafikiri ugomvi”basi tutacheeeka huku nikimpimia🤣🤣
 
😅😅😅yule mwanamke ni shida jaman.
Halafu alikuwa na short nails lakin😅😅akiniganda sasa🧚‍♀️🧚‍♀️Unaweza dhani umeng’ang’aniwa ma siafu

hahaha... polee

hivi hakukuachia alama kweli!?.....Hebu tuone!😜
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…