Leo ninajadili na maRasta: Je? Ulaji wa wadudu kama panzi, senene na mchwa ni sehemu ya ital?

Leo ninajadili na maRasta: Je? Ulaji wa wadudu kama panzi, senene na mchwa ni sehemu ya ital?

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2022
Posts
3,644
Reaction score
4,315
Wa gwaan, Jah Rastafarai, Selasie I King.
Wakush mpo? Ni amanii?

Swali hili linawahusu pia ma-vegetariano (sio ma-vegan), watu wote ambao kwa sababu zao na za ki-maadili hawali wanyama (ila wanatumia bidhaa zao kiasi) naomba wote mnijibu lakini haswa hawa marasta.

Kulingana na kanuni za ulaji na chakula bora kuna jamii zilizokuwa nazo hata kabla sayansi haijafika hapo.

Screenshot_20240915-132931_Chrome.jpg

Picha kutoka uzi wa Damaso Chapulines: Kitoweo cha Panzi kutoka Mexico

Mfano ni marastafari walioanza mudaa kufuatilia chakula chenye matunda na mbogamboga zaidi. Huku wakisisitiza matumizi madogo ya chumvi. Tumeona sayansi ineanza kushadadia haya mambo hivi karibuni tu.

Najua mnatumia na tunatumia maandiko mbalimbali kama msingi wa kanuni zetu na mwenendo wa kimaisha (lifestyle) basi ngoja nianze na hoja hizi:

1. Ili chakula bora kikamilike sehemu kuu ni protini na kabohaidrati na mengineyo ni kwa mbaali (madini, vitamini etc). Ndio maana hata biblia inaandika habari za maziwa (protini) na asali (kabohaidrati). Kutoka 3:8 “nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali.."

2. Rasta Yohana alipokuwa anaishi msituni aliipata protini yake kwa wadudu. Mathayo 3:4 Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.

3. Ulaji wa wadudu na ufugaji wao kiujumla ni endelevu na rafiki wa mazingira mno. Wanasayansi wamefanya tafiti na kugundua kuwa ulaji wa wadudu unaweza kuiokoa dunia. Uzaloshaji wa wadudu kwa chakula utaondoa utapiamlo na unatumia maji machache kuliko aina nyingine zote za vyanzo vya protini kama kuku na ng'ombe. Na rasta siku zote anapaswa kuyatunza mazingira na kuiheshimu asili.

4. Biblia pia imeandikwa waziwazi Walawi 11:20 “ ‘Wadudu wote warukao ambao hutembea kwa miguu minne watakuwa chukizo kwenu. 21Lakini wako viumbe wenye mabawa ambao hutembea kwa miguu minne mtakaowala: wale wenye vifundo katika miguu yao ya kurukaruka juu ya ardhi. 22Miongoni mwa hawa, mtakula nzige wa aina zote, senene, parare (crickets) au panzi."

Kwa hoja hizo hata kama nyama haipo katika ital ya marasta wengi (baadhi wanakula sana tu mfano nyama za porini) bado ufugaji ni kitu mkushi yeyote anaweza kufanya mfano;
A. Kufuga ng'ombe na mbuzi kwa ajili ya maziwa
B. Kufuga nyuki
C. ...............

Na tukijiuliza kwanza ni kitu gani kinafanya kuwala wanyama kuwa unyama, ni kuwakatili maisha yao. Lakini tujiulize kama ambavyo binadamu akifariki akiwa mzee sana inakuwa ni shangwe tu watu hawasikitiki sana zaidi wanashukuru kwa sababu siku zinakuwa zimefika.
Pia soma:
Je hatuwezi kutumia pointi hiyo hiyo?

Mfano kama kikawaida ng'ombe angeishi miaka 16 halafu akachinjwa akiwa amekomaa tu mfano miaka mitatu basi tunakuwa tumemkatili maisha yake. Labda ana mtoto mmoja tu na hajawaona wajukuu!😐.
Screenshot_20240915-123615_Chrome.jpg

Lakini ni vigumu kumleaa na kuja kumchinja akiwa na miaka 20 labda maana nyama yake haitakuwa nzuri tena.

Kwa mbuzi pia vile vile, mbuzi akichinjwa akiwa na mwaka mmoja anakuwa amekatiliwa miaka 10-15 hivi.

Sasaa tukirudi kwa wadudu, wapo baadhi (mfano nzige) ambao kwanza wakishataga mara moja tu tayari wametimiza ndoto zao duniani wanasubiri kufa tu. Je hawa ukiwala utakuwa umewakatili nini?

Na kumbikumbi nao weeeeeengi hufa/huliwa muda mfupi tu baada ya kuruka. Je ukiwala unakuwa umewakatili nini? Ninaweza kuelewa mfano mtu atakayemuwinda hadi kumla malkia wa kichuguu, huyu amemkatili maana angeweza kuishi hadi miaka 50. Na amewababaisha mchwa wengi sana lakini kuna uwezekano watampata mrithi wake mapema tu.
Screenshot_20240915-130058_Chrome.jpg


Anyway nisiongee sana, je? marasta kula wadudu ni sehemu ya ital (kanuni bora za chakula) au sio? Kama jibu ni ndio kwa nini na kama jibu ni sio kwa nini?

Na hata mavegetarian hili swali ni lenu, je kula wadudu ni vema au sio sawa? Kwa sababu gani?

-Emurasta!
 
Aman na Upendo
Kuna mstari kwenye Biblia (Agano la kale)Unasema Mwanamke atazaa kwa uchungu na Mwanaume atakula kwa jasho kwa kuitifua ardhi ya chini kuja juu na ya juu kwenda chini
So chakula wanaamin kitapatikana kupitia ardhi sio kuchinja.
 
Back
Top Bottom