mudy92
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 671
- 531
Wasalaam!
Miaka kadhaa nyuma nilijiunga na Jeshi la kujenga Taifa, nilipata mafunzo ya awali kwa muda wa miaka miwili kikosi fulani huko Nyanda za juu kusini.
Mwisho wa mwaka 2019 ulitokea ujenzi wa ukuta wa IKULU huko DODOMA na mimi nikiwa mmoja wa vijana nilioshiriki ujenzi huo pamoja na miradi mingine kama Hospital ya Uhuru, Uwanja wa Gwaride mpaka kupewa sifa ya Ushujaa na Ahadi ya Ajira na hayati Dr. John Pombe Magufuli baada ya kumaliza ujenzi.
Baada ya sekeseke la vijana kugoma na kulazimisha Ajira sikuwepo katika kundi hilo hivyo kubaki mpaka siku tuliyokwenda huko katika Kambi ya JWTZ kwa mafunzo ya Ajira.
Baada ya check up ya afya inayofanywa kabla ya kozi, niliandikwa kama UNFIT kwasababu ya usikivu hafifu wa sikio la kulia ambao sijui ulianzia wapi.
LEO hii nipo nyumbani baada ya Miaka 4 nikiwa sijui vipi nitaanza upya NAHISI KUPOTEA, sina wa kumlilia, Sina wa kumweleza inaniua taratibu na sijui KESHO ITAKUWA VIPI
Kinachouma Zaidi kuona mwenzio mwenye Shida kama yako ambaye hakushiriki ujenzi kwa miaka 2 akiendelea kuwepo katika Ajira wewe unarudi nyumbani, AJIRA zina MENGI wahanga ni WATOTO WA MASKINI.