Leo rasmi ligi kuu ya NBCPL inamalizika, mechi ipi utaitazama zaidi?

Leo rasmi ligi kuu ya NBCPL inamalizika, mechi ipi utaitazama zaidi?

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Ligi kuu ya NBCPL leo rasmi inatamatika kwa kucheza michezo nane na hadi sasa Bingwa ni Yanga lakini tutashuhudia vita vikali vya kumaliza nafasi ya pili ambapo hapa ni Simba sc na Azam fc ambao ndiyo wanao wanao wania nafasi hiyo

lakini vita nyingine ni ya mfungaji bora kati ya Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum wa Azam wote hawa wakiwa wamefunga magoli 18, nani kuondoka na kiatu?

Kivumbi kingine ni kutafuta nafasi ya kucheza playoff hapa ni Geita Gold na Dodoma jiji nani kumfuata Mtibwa Sugar ambaye kashashuka ligi rasmi.
 
Nitaitazama mechi ya Azam vs Geita.
Azam leo hapati ushindi.
Simba anashinda anachukua nafasi ya pili,
Ndo mtaelewa kwamba Azam na Simba ni team 1
 
Nasubiri UEFA Euro 2024 kuanzia June 14, sitazami game yoyote leo sioni ya maana.
 
Game ya Azam na Geita ni mguu wa shingo mguu wa roho itakuwa tough sana
 
Back
Top Bottom