Kipala
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 3,763
- 700
Leo hii tar 21 Desemba ni siku ndefu ya mwaka, ni siku ya solistasi. (Waingereza husema solstice) .
Leo Jua linafika nafasi ya kusini zaidi hivyo iko juu zaidi angani. Na njia yake kwenye anga ni ndefu kushinda siku zote hivyo wakati wa mchana ni ndefu kidogo.
Ilhali Tanzania iko karibu na ikweta tofauti si kubwa vile; pale Nairobi karibu haionekani na Nanyuki hamna kwa sababu iko ikweta penyewe.
Kinyume chake upande wa kaskazini wa Dunia siku ni fupi hivyo usiku ni mrefu. (Hapa ni pia sababu ya sherehe ya Krismasi kutokea siku hizi - maana watu wa kaskazini waliona hadi leo giza limeongezeka tangu Juni, lakini kuanzia kesho giza linapungua tena)