Leo Tarehe 26-02-2025: Imetimia miaka 140 Tangu kufanyika kwa Mkutano wa Berlin

Leo Tarehe 26-02-2025: Imetimia miaka 140 Tangu kufanyika kwa Mkutano wa Berlin

Kinyungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2008
Posts
19,484
Reaction score
38,416
20250226_162929.jpg

Miaka 140 iliyopita tarehe kama ya leo ndipo mkutano wa Berlin ulipohitimishwa. Mkutano ulianza Tarehe 15 Novemba 1884 na kuhitimishwa Tarehe 26 Februari 1885 kwa kusainiwa kwa makubaliano ya jumla baina ya mataifa yaliyoshiriki.

Jambo la kustaajabisha kwenye mkutano huu ni kuwa ingawa Marekani nayo ilishiriki mkutano huu lakini ilikuwa na haki ya kipekee ya kukubali au kukataa maamuzi ya Mkutano huo. Marekani haikusaini makubaliano ya mkutano huo yanayojulikana kama "Geneal act" ambayo nakala yake imeambatanishwa hapo chini

Jambo lingine la kipekee ni kwamba Sultani wa Zanzibar alitaka sana kualikwa kushiriki mkutano huo lakini Waingereza walicheka wazo lake la kutaka akaribishwe na hatimaye hakualikwa

Mwenyekiti wa mkutano alikuwa ni Kansela wa Ujerumani, Otto von Bismarck. Mkutano huu ulilenga kuweka kanuni za kugawana Afrika kati ya mataifa ya Ulaya ili kuepuka migogoro yao ya kikoloni.

Mataifa hayo yaliamua kwamba nchi yoyote iliyotaka kudai sehemu ya Afrika ilipaswa kuwa na uwepo wa kudumu na kuonyesha maendeleo ya kiutawala. Matokeo ya mkutano huu ni kugawanywa kwa bara la Afrika bila kuzingatia mipaka ya asili ya makabila na mataifa ya Kiafrika.

Nchi Zilizoshiriki:

1. Ujerumani
2. Uingereza
3. Ufaransa
4. Ureno
5. Ubelgiji
6. Hispania
7. Italia
8. Uholanzi
9. Denmark
10. Uswidi-Norway
11. Austria-Hungary
12. Urusi
13. Marekani
14. Milki ya Ottoman


Kabla ya mkutano huo 80% ya ardhi yote ya Afrika ilikuwa chini ya milki ya wazawa wa bara hilo, wageni wakiwa wameshikilia maeneo machache ya pwani ya Afrika. Hata hivyo kufikia mwanzo wa vita ya Kwanza ya Dunia ni mataifa ya Ethiopia na Liberia tu yaliyosalia na uhuru wake katika bara zima la Afrika

Wiki moja kabla ya kufungwa kwa mkutano huo, gazeti moja la huko Nigeria la Lagos Observer liliandika kuwa "huenda dunia haijawahi kushuhudia wizi wa kiwango kikubwa kama hiki."

Miaka sita baadaye, mhariri mwingine wa gazeti hilo hilo la Lagos Obsever, alilinganisha mkutano huo na urithi na biashara ya utumwa, kwa kusema: "Umilikaji wa ardhi yetu kwa nguvu umechukua nafasi ya umilikaji wa miili yetu kwa nguvu."

Theodore Holly, Askofu wa kwanza mweusi wa Protestant Episcopal Church nchini Marekani, aliwalaani wajumbe wa mkutano huo kwa kusema kwamba walikuwa wamekusanyika "kutunga sheria za unyang’anyi wa kitaifa, wizi na mauaji."





 

Attachments

Mambo ya kijinga kabisa, tulitakiwa tuyatoe kwenye historia yetu, AU igawe afrika kwa kufuata ethic groups maisha yaendelee
 
Back
Top Bottom