Leo tarehe 28 mwezi Septemba ni siku ya kichaa cha mbwa duniani, tujikumbushe kuhusu ugonjwa huu hatari

Leo tarehe 28 mwezi Septemba ni siku ya kichaa cha mbwa duniani, tujikumbushe kuhusu ugonjwa huu hatari

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
images (37).jpeg

Kichaa cha Mbwa ni ugonjwa hatari unaosababishwa na kundi la virusi waitwao Lyssa (kuna virusi wa Rabies na virusi wa Australian bat wote hawa huleta ugonjwa huu).

Ugonjwa huu huwapata binadamu kwa kuumwa na mnyama Kama Mbwa, Mbwa mwitu, paka, Fisi, popo na wengineo wa jamii hiyo mwenye virusi hawa wa lyssa.

Binadamu pia anaweza kuambukizwa kwa kugusa au kuingiwa na mate ya mnyama aliyeathirika, kupitia jeraha, mchubuko, jicho, pua au mdomo, hivyo usipuuze hata huyo mnyama atakapo kusababishia mikwaruzo tu .

Virusi hawa wanapoingia mwilini kwa mtu huenda hadi kwenye ubongo kupitia mzunguko wa damu ambapo huanza kuleta mashambulizi katika mishipa ya mfumo wa fahamu mpaka mtu kufikia hali ya kichaa cha Mbwa.

DALILI ZA KICHAA CHA MBWA
Inamchukua mtu siku kadhaa mpaka hata miaka kadhaa kuanza kuonesha dalili za kichaa cha Mbwa.

Ina tegemea pia sehemu ya jeraha la kung’atwa ilipotokea. Kwa mfano aliyeng’atwa sehemu ya kichwa au shingo ataonesha Dalili mapema zaidi kuliko aliyeng’atwa miguuni. Lakini muda wa wastani wa dalili kuanza kuonekana ni mwezi 1 hadi 3. dalili hizo ni kama zifuatazo:-

1. Homa na kuhisi uchovu mwa mwili.

2. Kuumwa kichwa

3. Kuchanganyikiwa

4. Kubadilika tabia kuwa mkali kupita kiasi

5. Kukasirika au kuogopa sana

6. Kuogopa Mwanga 'photophobia'

7. Kuogopa maji ‘hydrophobia’, hasa kunywa

8. Kukosa uwezo wa kutawala mwendo wa viungo vya mwili

9. Kupoteza fahamu

Soma Pia: Dar es Salaam yaongoza kwa Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa Tanzania

Mara dalili hizi zinapoonekana maana yake ugonjwa umeshaanza kuharibu ubongo na neva na uwezekano wa mgonjwa kupona kunakuwa ni nadra sana na hivyo basi kifo huweza kutokea.

MATIBABU NA KINGA
1. Kusafisha jeraha

Endapo mtu atang’atwa na Mbwa au mnyama mwingine yoyote, aoshe sehemu ya jeraha kwa maji mengi yanayotiririka na sabuni kwa angalau dakika 15Kidonda kisifungwe na mhanga apelekwe hospitali au kituo cha Afya kupatiwa chanjo ili kuzuia madhara dhidi ya kichaa cha Mbwa.

Unaweza tumia maziwa pia kama maji hakuna.

2. Rabies ImmunoGlobulin (RIG) hizi kinga zitatolewa kwa jeraha linalotoa damu.

3. Chanjo kwa aliyepata jeraha na wanyama tunaoishi nao

Tiba ya chanjo kujikinga na maambukizi ya virusi hivi ikitolewa mapema au mara moja baada ya kuambukizwa, lakini tiba inahitaji kutekelezwa kabla virusi havijafikia ubongo, kwa hiyo ni muhimu kupata matibabu katika muda wa saa za kwanza baada ya kung’atwa. Idadi ya Chanjo inategemea kama mbwa au Mnyama aliyekung'ata amepata chanjo au la .

Pia ni muhimu kutoa chanjo kwa mbwa wote ili kuwakinga na virusi hivi.

MWISHO: Ni vizuri ukipata chanjo mara tu baada ya kung’atwa Na Mnyama kabla hujaonesha dalili zozote kwani ugonjwa huu hauna tiba.

Lakini pia ni muhimu wanyama wa kaya wapewe chanjo dhidi ya ugonjwa huu ili kulinda mbwa kutopata maambukizi ya virusi hivi.​
 
Wanasema dalili zikishaanza kuonekana hakuna uwezekano wa kupona.

Nimeshtuka kujua kwamba hata paka ana uwezo wa kusambaza huu ugonjwa! Nyumbani watoto mda wote wanacheza na paka na kuna wakati paka wanawakwaruza kwa makucha yao
 
Back
Top Bottom