Leo terehe 21 01 2023 Uhuru wa Tanganyika!

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Leo ni siku muhimu sana katika historia ya Tanzania siku ambayo watawala wamewapa watawaliwa Uhuru wa kupaza sauti zao, mkoloni wa kiingereza hakuwahi kuwafunga midomo watanganyika kupaza sauti zao kudai Uhuru, waliodai Uhuru hawakufanywa lolote kwani ilikuwa ni haki ya watanganyika kudai Uhuru na hii ni tofauti baada ya kuingia watawala wenyeji.
SHIME WANANCHI TUIJENGE NCHI YETU KWA PAMOJA.
 
Ndio maana Hayati Mkapa aliwaita Wapumbavu na malofa ,nikajua mngebadilika kumbe bado ule ututusa mnao
Mpumbavu na lofa ni yule asiyejua haki zake za msingi katika maisha, ndiyo sababu Mkapa akagawa mali za wananchi kwa watu binafsi akikoleza ufisadi huku akijua watanzania tutakula nyasi kwani tumelala.
 
Umepotea kamanda ila hujachelewa bado kuzirudia akili zako. Hata hao mnaotaka kuwaonesha Tanzania hakuna Uhuru wanatambua na wanafahamu Tanzania ni Taifa huru kimawazo na kifikra.
 
Umepotea kamanda ila hujachelewa bado kuzirudia akili zako. Hata hao mnaotaka kuwaonesha Tanzania hakuna Uhuru wanatambua na wanafahamu Tanzania ni Taifa huru kimawazo na kifikra.
Tatizo lako ni uelewa mdogo, kabla ya kukurupuka ungesoma vizuri na kuelewa kisha ungeandika badala ya kuandika bila ya kusoma na kuelewa.
 
Upumbavu ni kuminywa haki zako kisha unakaa kimya mpaka alikuminya akufanyie hisani
Ndivyo watanzania wanavyopenda, kuna mtanzania amelazimishwa kupigana vita kwenye jeshi la Urusi na ameuawa, watanzania tuko kimya, serikali iko kimya! Dunia inatushangaa.
 
Ndivyo watanzania wanavyopenda, kuna mtanzania amelazimishwa kupigana vita kwenye jeshi la Urusi na ameuawa, watanzania tuko kimya, serikali iko kimya! Dunia inatushangaa.
Pengine hujaandika wewe hii mada lakini kama umeandika rudia kusoma ulichoandika pengine ulikituma bila kujua. Umeandika hivi leo 21.01.2023 ni siku ya Uhuru wa Tanganyika, narudia tena acha ututusa Tanganyika ni huru .

Umezungumzia juu ya ukoloni lakini kwa kiasi fulani naona kama umepotosha. Harakati za mtanzania kujikomboa hazijaanza kwa Mwalimu, zipo toka Kipindi Cha mkutano wa Berlin 1884-1885 ambapo Afrika ikaanza kutawaliwa na wakoloni na Tanzania pia.

Katika harakati za ukoloni kututawala, kuna vita mbalimbali zilipiganwa kupinga hilo. Mfano mkubwa ni Vita ya wahehe na wajerumani na harakati za kujikomboa zikaendelea mpaka vita vya majimaji.

Haya yote yalikuwa ni katika kupinga ukoloni.

Baada ya Uhuru ,Tanganyika na baadae Tanzania iliondoa mazingira yote na makovu yaliyotokana na ukoloni na matokeo yake ni amani ,mshikano uliopo mpaka sasa.

Anapotokea mtu na kudai leo ni siku ya Uhuru wa Tanganyika napata mashaka sana na zaidi anapotokea mtu na kusema bora wakoloni ni Jambo la ukichaa, hata Kama watanzania ni wepesi wa kusahau si vema tukasahau machozi ,jasho na damu la wazee wetu katika kutuletea uhuru
Tatizo lako ni uelewa mdogo, kabla ya kukurupuka ungesoma vizuri na kuelewa kisha ungeandika badala ya kuandika bila ya kusoma na kuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…