Mario Kejob
JF-Expert Member
- Apr 14, 2020
- 441
- 536
Leo TRA wamepita mitaa ya Manzese na kuwataka wenye maduka bila kujali ukubwa wa duka kuweka EFD machine na kuwalazimisha wafanya biashara kusaini form za kukubali kuweka hizo EFD katika kipindi kisichozidi siku tatu.
Miongoni wa waliolazimishwa kusaini form hizo ni pamoja na saluni, barbershop,viduka vya uchochoroni na hata baadhi ya mama ntilie wenye frame.
Wadau hili limekaaje? Ninavyoelewa mimi ni maduka yenye mtaji wa zaidi shilingi milioni tano na si kila duka au kila frame. Au serikali ilitoa waraka mwingine wa kufanya hivyo? Nimeambiwa hizo EFD huuzwa shilingi laki nane na wenye viduka hivyo sidhani kama hizo pesa wanazo.