Leo tunafunga rasmi mjadala kwa Kukubaliana kuwa ni kweli kabisa Wanawake wote Kipaumbele chao kwa Wanaume ni Pesa na Maisha mazuri na siyo Mengineyo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Akiwa mfanyakazi wa Redio Berlin Internation nchini Ujerumani, James Lembeli alikutana na binti wa Kijerumani, Birgit Lifka, wawili hawa wakaanzisha urafiki uliowapeleka kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Kwa Lembeli uhusiano huo haukuwa wa kupoteza muda, aliamini kuwa mwanamke huyo ndiye atakayekuja kuwa mke wake na mama wa watoto wake kwa kuwa alishamridhia kwa shida na raha.

Wakati yeye akiwaza hivyo, mambo yalikuwa tofauti kwa Birgit, yeye alitaka uhakika wa maisha yake, hilo lilimfanya akatae kuja Tanzania kuishi na mwanamume huyo kwa kuwa hakuona hatima yake siku za usoni.

Katika mahojiano aliyofanya na gazeti hili, Lembeli anasimulia kisa hicho akikumbuka namna umaskini ulivyomfanya amkose mrembo huyo wa Kijerumani.

Mwanasiasa huyo mkongwe, mbunge wa zamani wa jimbo la Kahama mjini, anasema kutokuwa na kazi kuliharibu ndoto hiyo, ingawa baadaye alikuja kumpata mke wa maisha yake, Hawa Mchinja.

"Ni 'binti' mrembo wa Kimasai kutoka Arusha, alibadilisha maisha yangu kabisa, nilipomchumbia ikabidi nimwambie yule wa Ujerumani kwamba sasa nataka kuoa.

"Aliniandikia barua ya kurasa tisa, kilichoandikwa mule ni siri yangu," anasimulia Lembeli, katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika Julai Mosi, jijini Dar es Salaam yakiangazia masuala mbalimbali ya kisiasa na kijamii.

Chanzo: mwananchi_official

Jidanganye tu hapo ulipo kuwa hata kama huna Hela basi Mwanamke atakupenda na kukuvumilia Maishani sawa?

Kudadadeki......!!
 
ni kweli ila aliyezidi mnyama nguruwe wa kike yani mapenzi yake ni msosi
 
Okay, umeshajua yeye anataka pesa wewe kwake unataka nini??
Bora yake anajua atakacho, itakua mbaya kwako kama umejua anataka pesa na wewe hujui unataka nini, ama lah unataka kitu asichoweza kuoffer.

Mpe pesa akupe utakacho, kama hawezi huyo hakufai, na kama huwezi basi wewe pia humfai.
 
Heshima ya mwanaume kwa mwanamke ni pesa tu sio kitu kingine
 
kuna kamoja kananidanganya nikalipie ada kananiambia mimi mwanaume wa maisha yake. nikakaambia kwenda huko nikusomeshe uwe na elimu wakati mm mbeba tofali ukishaipata hiyo elimu si utataka wasomi wenzio. nikakatimua
 
Ukweli mtupu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…