Video haifunguki, lakini naamini huyu mzee alikuwa anafanya kweli, japo yapo makosa aliyoyafanya kama binadamu, lakini kwa kiasi kikubwa alijitahidi sana kuijenga tz ya kujitegemea, alisema...NCHI HAIWEZI KUWA HURU KAMA BADO NI TEGEMEZI KIUCHUMI...na kweli leo ndio tunachokiona, tuna UHURU wa bendera tu, lakini kila kitu kinakuwa controlled kutoka mataifa makubwa, na rais wetu bila aibu, kutwa kucha kutembea kama YATIMA KUOMBA OMBA NCHI ZA NJE...ilihali tuna rasilimali chungu nzima....KIKWETE ANATUABISHA SANA KAMA TAIFA.