LEO: Wabunge nchini Uganda wapigana ndani ya ukumbi wa Bunge

LEO: Wabunge nchini Uganda wapigana ndani ya ukumbi wa Bunge

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Wabunge nchini Uganda wamepigana ndani ya ukumbi wa bunge wakiwa katika siku ya pili ya kikao cha kujadili wa muswada wa kuondoa ukomo wa miaka ya kugombea nafasi ya urais kwa mjibu wa katiba ya taifa hilo.

Ugomvi huo ulianza pale Spika alipochukua hatua ya kuwafukuza wabunge wapatao 25 wengi wao wakiwa ni wale wa upinzani kwa madai ya utovu wa nidhamu pamoja na waziri wa serikali aliyeshtakiwa kwa kufyatua risasi bungeni siku ya Jumanne.

Hata hivyo Wabunge wa chama tawala nchini Uganda wamefanikiwa kuwasilisha ombi la kuandaa mswada wa kubadilisha katiba na kuondoa kifungu kinachozuia mtu kuwania urais akiwa na umri wa zaidi ya miaka 75.

Wabunge hawa wanadai kuwa kama kikomo cha umri wa miaka 75 kitaondolewa basi rais aliyepo kwa sasa atapata mwanya wa kugombea tena mwaka 2021.

pi3.jpg




ITV
 
system ya huko imepigwa ganzi? kama mtu ni national threat si wamueliminate tu kwani alizaliwa ili awe raisi miaka yote?
 
Back
Top Bottom