Leo wabunge wanakwenda moja kwa moja kwenye point hakuna kupongezana wala kupeana pole, Kilango alia na upendeleo!

Leo wabunge wanakwenda moja kwa moja kwenye point hakuna kupongezana wala kupeana pole, Kilango alia na upendeleo!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mjadala wa ofisi ya Rais Tamisemi unakwenda vizuri ile mambo ya kusifia sifia kutoa pongezi na pole haipo leo.

Mbunge wa kwanza kuchangia Anna Kilango ametaka majimbo yote yaangaliwe kiusawa kwenye swala la fedha za maendeleo badala ya fedha kupelekwa jimbo moja tu kwa upendeleo.

Amesema wilaya ya Same ina eneo la 40% ya mkoa wa Kilimanjaro lakini ndio inapata fedha kidogo kuliko wilaya zote.

Ramadhan Kareem!
 
Huyu Mama ni mbunge wa miaka mingi sana kwenye nafasi ya Ubunge wa jimbo na viti maalaum kupitia nafasi 10 za Rais. Tatizo hilo alikuwa hajaliona miaka yote hiyo?
 
johnthebaptist ,

kilango na mathayo ni kikwazo cha maendeleo ya wilaya ya same. wilaya ya same inahitaji damu mpya katika nafasi za wabunge. changamoto za wilaya ya same tulishazijadili miaka mingi hapa jamii forums.

Wananchi walichagua mbunge wa upinzani lakini akaishia kuhujumiwa na chama tawala. kuna wakati mawaziri walikuwa wanatoa majibu ya uongo kwa maswali yaliyoulizwa, na kero zilizokuwa zikiwasilishwa, na mbunge wa same mashariki na rekodi hizo ziko kwenye hansard ya bunge.

 
angalau sku hz naskiliza bunge na pia naskiliza taarifa ya habari. hapo nyuma nilikua nakereka sana kusikiliza bunge mana mbunge anawasha maik afu anatumia dakika 10 kumsifia magu,dakika mbili kuongea umbeya,dakika 3 kumshukuru supika. afu anakaa yaan nlikua nakereka sana asee.
 
Back
Top Bottom