Leonard Rwizandekwe: Mtanzania pekee aliyethubutu kumuondoa Nyerere madarakani Kikatiba

Kuna watu walikuwa wanamwona mwalimu ni dikteta lakini huyu mtu alimpinga na hakumfanya chochote wengine wanasema aliwakandamiza waislamu lakini huyu kathibitisha kuwa shule zilitaifishwa ili kuweka mizani sawa ya wakristo na waislamu kupata elimu sawa wale wa propaganda karibuni sana
 
Very splendid aisee
 
Huyu mzee alikua kichwa sana na aliandika mambo ya msingi. Kuhusu waislam wenzetu, wengi walifundishwa kwamba elimu dunia haina maana so madrasa ndio kila kitu na hayo mawazo kijijini bado yapo. Kaka yangu ni muislam lakin anathamin sana elimu, ila mke wake alisababisha watoto wake wasisome eti wanapoteza muda kwenda kusoma shule za wakristu wakati ni shule za serekali. Kingine shule nyingi zinazomilikiwa na tasisi za kiislam hazifanyi vizuri kwenye mitihani nahisi kwa sababu nadhani vipindi vya dini vinachukua muda mwingi, lakin pia ule msisitizo wa kuwambia watoto wajue jinsi ya ku balance vyote unakua hakuna.
 
Huyo Wa matofali ni yupi mkuu?!
 
Huyu mzee bado yupo mwaka jana nilipokuwa kwenye msiba wa mzee Kikenya hapo Kiziba. Alikuwa kivutio.
Sasa vyombo vyetu vya habari wazee kama hawa ndio wakufanya nao vipindi watupe mambo mengi na historia za kutukuka Kwa taifa letu,,, sio kila kukicha ni interview na wasanii Wa bongo flavor,,, shenzy kabisa!
 
Shule nyingi za kiislamu zinakosa uongozi mzuri, wengi wa wazazi hupenda watoto wao wasome bure, matokeo yake hawapati walimu wazuri, kwasababu ya kupata changamoto ya ulipaji wa mishahara
 
Hilo andiko na hiyo aina ya kiswahili kilivyoandikwa kama ni halisi nampongeza sana huyo aliyetamani kugombea urais.

Hii ina dhihirisha kuwa siyo kweli kuwa eti mmoja tu ndo ana stahili na bila yeye hakuna mwingine.
 
Huyu mzee ni kichwa maana Ilani yake bado relevant mpaka leo. Halafu hakuwa mbaguzi kama aliguswa na kutokusoma kwa waislam kweli nimmtu aliyetaka maendeleo yanchi kwa ujumla wake
Hizi habari Ni nzuri lakini validity yake inatia shaka.Anataja kuasisi jambo fulani bila ushahidi hata kututajia aliokuwa nao hasemi zaidi ya kumtaja mwalimu.Anataka tuamini kwamba kila zuri alilolifanya Nyerere aliliasisi yeye na ushahidi hakuna.Hebu tumuulize,wakati wa uasi wa jeshi mwaka 1964 yeye alikuwa wapi? Na je ,wakati Nyerere na Kambona wanasigana juu ya Azimio la Arusha,yeye ambaye Ni muasisi kwa madai yake alikuwepo Arusha? Kama alikuwepo Arusha,alikuwa upande upi kati ya pande hizo mbili?
 
mzee alikua kichwa ila tatizo inshomire mwalimu aliwajua hii inchi ingetawaliwa na wahaya hadi mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…