Ezio Ezio
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 423
- 666
Salamu wana jf,
kutokana na kupenda sana historia za kale ( ancient history) nimekua nikifuatilia stori mbali mbali na ningependa kushiriki na ninyi katika hii. Hii ni mara ya kwanza kuandika stori hivyo naomba kuvumiliwa kwenye mapungufu ambayo yatajitokeza. Kwenye stori hii nitajaribu kuelezea yafuatayo
• Leonidas ni nani?
• maisha yake yalikuwaje?
• kwa nini anakumbukwa katika historia za kale?
Leonidas alikuwa mfalme wa 17 wa jiji la Sparta kutoka Greek ( ancient Greece), na asili yake ni kutoka katika ukoo wa kina Agiad (Agiad dynasty) .Alizaliwa 540BC huko Sparta na alifariki mwaka 480BC kwenye mapambano ya vita huko thermopylae. Leonidas maana yake ni mtoto wa simba.
Alizaliwa katika familia ya kifalme akiwa mtoto wa 3 kuzaliwa. Baba yake alikuwa mfalme Anaxandridas II wa Sparta. Mfalme Anaxandridas II alimuoa mtoto wa kaka / dada yake (niece) ambae ndie mama yake Leonidas. Hiyo ilipelekea mfalme Anaxandridas II kushauriwa kumuacha mkewe sababu ya undugu ila alikataa kata basi ikabidi ashauriwe kuoa mke mwingine pasipo kumuacha yule wa kwanza (ndugu yake). Mke wa pili baada ya kuolewa alizaa mtoto wa kwanza (prince) na aliitwa CLEOMENES. Baada ya mwaka 1 mke wa kwanza nae akazaa mtoto wa kiume akaitwa DORIEUS.
Leonidas alikuwa mtoto wa pili wa mke wa kwanza wa mfalme Anaxandridas II na inasemekana alikua na pacha CLEOMBROTUS. Japo kuna taarifa nyingine kuwa Leonidas na cleombrotus hawakuwa pacha ila walipishana mwaka kuzaliwa.
Kwa sababu Leonidas hakuwa mrithi wa kiti cha ufalme kutokana na utaratibu wa kuwa mtoto wa kwanza ndie hurithi kiti cha ufalme, ilimpasa kuhudhuria shule za kawaida ( public schools) ambako watoto wa raia wa sparta wanashindana au kupigania haki ya kuwa raia wa sparta. Hivyo Leonidas alikuja kuwa mmoja wa wafalme wa Sparta wachache sana kupitia mafunzo hatari na magumu kabisa ya kijeshi / upiganaji (warrior) ya Sparta.
Kati ya mwaka 516 BC - 520 BC, Cleomenes alikuwa mfalme baada ya baba yao kumuachia madaraka, kitu ambacho kilipelekea kaka yake Leonidas (DORIEUS) kukasirika sababu alitaka yeye awe mfalme wa Sparta, inasemekana DORIEUS aliondoka kuja Africa kuanzaisha makoloni na baada ya kushindwa alielekea Sicily amabako alifia huko.
Leonidas nae alimuoa mtoto wa kaka yake ( cleomenes) aitwae Gorgo. Mnamo mwaka 490/491 BC taifa la persia lilijaribu kuivamia Greece kwa mara ya kwanza na kukutana na upinzani mkali, kipindi hicho hicho cleomenes aliondolewa madarakani kwa kigezo cha kupatwa na ugonjwa wa akili (insanity) na mnamo mwaka 489BC Leonidas akawa mfalme wa Sparta.
Umaarufu wa Leonidas unakuja zaidi pale ambapo taifa la persia chini ya mfalme wao Xerxes waliivamia Sparta kwa mara ya pili mwaka 480BC na ndipo jina la vita/mapigano ya thermopylae ( battle of thermopylae) lilizaliwa. Labda nieleze thermopylae ni nini?
Thermopylae ni jina la eneo ambapo mapigano maarufu yalifanyika, neno thermopylae kwa kiingereza linamaana "hot gates" kutokana na eneo hilo kuwa na chemi chemi zinazotoa maji ya moto na wenyeji waliamini kuwa hapo kuna mlango wa kuingia kuzimu ( kwa mungu wa kuzimu Hades, mtoto wa Cronus na Rhea, ambapo Hades alikua na kaka wawili ambao ni Poseidon na Zeus, hii ni kwa mujibu wa imani ya zama za kale za Greece) . Hiyo ndio asili na maana ya thermopylae au malango ya moto ( hot gates) .
Katika vita hii ya thermopylae ni kwamba taifa la persia lilituma mjumbe kutaka Leonidas na Sparta wajisalimishe ( surrender) ambapo majibu yalikua ni kumuua na kumtupa kisimani yule mjumbe kutoka persia. Mfalme Leonidas akaona kuliko kungoja wafike ni heri kwenda kuwapokea huko huko ( kupambana nao kabla hawajaingia Sparta) na sehemu nzuri ilikua ni eneo la thermopylae kutokana na jiografia ya eneo husika kuwa na milima mikubwa miwili iliyoacha njia nyembamba katikati na hapo aliona ndio atapopambana kufa na kupona yaani ile wanasema last man stand.
Kabla ya kuondoka mfalme Leonidas alienda kuuliza kwa oracle ( mkuu wa kidini / imani fulani na inaamimika walikua na uwezo wa kutabiri) juu ya matokeo ya hii vita. Oracle alikataa asiende akitabiri kuwa ataangamia kwa kusema taifa litamlilia mfalme wake.
Inasemekana tarehe 4 mwezi wa 8 mwaka 480 BC mfalme Leonidas alitoka Sparta kwenda kukutana na majeshi ya mfalme Xerxes katika eneo la malango ya moto ( thermopylae) akiwa na jeshi dogo la wanajeahi 1200 ( 900 wakiwa ni muungano wa majeshi ya miji mingine na 300 jeshi la Sparta) huko mbele aiungana na majeshi mengine zaidi na kufikia idadi ya watu 7000. kule thermopylae walienda kukutana na jeshi kubwa toka kwa adui wao mfalme xerxes ambapo alikua na jeshi la watu kati ya 70,000-300,000.
Xerxes alingoja kwa muda wa siku 4 akiamini jeshi la Leonidas litaogopa na kuamua kusalimu amri na kuweka chini silaha zao. Kitu ambacho upande wa pili Leonidas alikua hata hawazi kuja kusalimu amri, kwake huo msamiati haupo kabisa.
Hatimae kuanzia siku ya 5 jeshi la persia likaanzisha rasmi mapigano ambayo yalidumu hadi siku ya sita huku ile mistari ya mbele ya jeshi la persia ikishindwa vibaya mno na inakadiriwa hadi kufika hapo zaidi ya wapiganaji 10,000 wa persia walipoteza maisha. Hata kile kikosi hatari zaidi cha persia kilichojulikana kama the immortals nao hawakufua dafu, walishindwa vibaya sana na kupeleka ndugu wawili wa mfalme Xerxes (Abrocomes na Hyperanthes) kuuwawa katika mapambano yale.
Siku ya 7 ( tarehe 11 / 8 / 480 BC) alikuja mtu mmoja raia wa Greece aliyeitwa Elphialtes kutoka jiji la Malian ambae aliwasaliti jeshi la Greece. Wakati Elphialtes anakuja na jeshi la persia lililokua likiongozwa na mkuu wa majeshi Hydarnes kupitia upande wa nyuma ( baada ya kuwaonesha jeshi la persia njia ya siri tofauti na inayolindwa na mfalme Leonidas wakati huo) hapo mfalme Leonidas alikua amewaruhusu kuondoka sehemu kubwa ya jeshi lake na kubaki na jeshi dogo la watu 1900 tu ambao waligoma kata kata kuondoka uwanja wa mapambano. Kati ya waliobaki 300 walikua Spartans, 700 thespians na 900 helots.
Inaaminika kuwa mfalme Leonidas aliamuru wapiganaji wake waondoke kwa sababu aliona ni vizuri kubakiza jeshi la akiba endapo kutatokea uvamizi sehemu nyingine kutoka kwa Xerxes na watu wake. Alitambua fika hakuna mtu wa Sparta hata mmoja ambae angekubali kuondoka eneo la mapambano hivyo alidhamiria kubaki na hao wanaume 300 wa Sparta kuhakikisha hapiti mtu hapo wakati huo wale wanaorudi waondoke eneo la mapambano salama. Ndipo hayo makundi mawili nayo yakagoma kumuacha Leonidas peke yake na Spartans wake 300.
Sasa basi baada ya yule msaliti Ephialtes kuja na jeshi lingine kutokea upande wa nyuma mfalme Leonidas na wapiganaji wake wakawa wamezingirwa pande zote, hata baada ya kupewa nafasi ya kusalimu amri na Xerxes bado shujaa huyu mtu wa Sparta alikataa na kuamua kupambana mpaka mwisho. Kutokana na uchache wa wapiganaji wa mfalme Leonidas waliobaki hakichukua muda mfalme wa persia kupata ushindi, wale Spartans 300 wote na mfalme Leonidas walifia pale, wale 700 Helots pia wote walifia pale na katika wale thespian 900 ni 400 tu ndio walipona baada ya kusalimu amri.
Wakati bado wapiganaji wa mfalme Xerxes wamelewa sifa ya ushindi inasemekana wale wapiganaji walioruhusiwa kurudi walipeleka taarifa Sparta na hivyo kupelekea wapiganaji kutumwa wakatoe msaada maana ilikua ni bora kufa kwa mpiganaji wa sparta lakini sio kumuacha mpiganaji mwingine vitani. Jeshi hili la pili lilifika kwa nguvu ya ajabu na kufanikiwa kulirudisha nyuma mara 4 zaidi jeshi la persia. Walifanikiwa kuupata pia mwili wa mfalme wao mpendwa Leonidas kabla haujachukuliwa na mfalme Xerxes ambae alidhamiria kukata kichwa cha Leonidas na kuweka kwenye mti kama ishara ya ushindi.
Kwa wapenzi wa movies nadhani wanaijua 300 muigizaji mkuu akiwa Gerald Butler akiigiza kama mfalme Leonidas, japo kuna mengine yaliongezwa kama wale wazee wa sparta kupewa hela na Xerxes na pia kwenye kipande cha mabishano kwenye baraza la mashauri lakini ni filamu inayoelezea vizuri mapigano haya ya malango ya moto ( BATTLE OF THERMOPYLAE ).