Leseni mbili za biashara kwenye ofisi moja

encyclopaedia Tanzaree

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
515
Reaction score
405
Habari wakuu, kutokana na hali ya biashara kuwa ngumu imetulazimu baadhi ya wafanyabiashara kufanya biashara zaidi ya moja kwenye jengo moja ili kuongeza kipato na kupunguza gharama za uendeshaji.

Jambo hili linatuweka matatani baadhi yetu kwa kugombana sana na watu wa leseni wakidai kwamba kila biashara inapaswa kuwa na leseni yake.

Mfano una duka la nguo kama major business ukaamua kuongeza uwakala wa mitandao ya simu kama minor business, watu wa leseni wakipita ukawa onyesha leseni ya duka la nguo bado watakudai leseni ya Mobile Money. Hii imekaaje ukizingatia tunapoomba uwakala tunaambiwa tutumie leseni ya biashara yoyote?

Upande wa uwakala wa benki wanasema ili wakupe uwakala basi huo uwakala usiwe ndio biashara yako kuu.

Hawa watu wa leseni wapo sahihi kudai leseni mbili ndani ya fremu moja hata kama hujaweka partitions?

Nawasilisha.
 
Kisheria Wako Sahihi. Leseni inalenga biashara na sio Premise.Hata hivyo kutegemea aina ya biashara ambazo unafanya unaweza kuomba aina flani za leseni ambazo ni more inclusive. Cha muhimu ni kuhakikisha kwamba aina ya biashara unayofanya inakuwa ndani ya leseni yako.
 
TRA wameshaacha kufanya kazi kwa weledi bali wanafanya kazi kwa kukomoana........wanatafuta kila mwanya wa kupata rushwa......

Fuata muongozo wa leseni yako mkuu....uwe makini maana wengine wanakuwaga matapeli.....kabla ya maongezi yoyote na mtu usiyemfahamu kwanza dai kitambulisho cha huyo mtu.....
 
TRA hawahusiki na leseni.Tra wanaangalia GROSS Sales zako wanadai chao.License ni BRELA or via Halmashauri.Ni muhimu sana mtu ajitambulishe hasa anapofuatilia masuala ya kiserikali maana ni kweli utapeli ni mwingi sana zama hizi.
 
Tuseme TRA wanashindwa kukaa vizuri na watoa huduma hizo za uwakala kurahisisha mambo maana terms zao kama vile zinapingana.
 
Ubarikiwe sana mkuu.....bahati mbaya ni wananchi wachache sana wanaoyajua hayo.......
 
TRA wameshaacha kufanya kazi kwa weledi bali wanafanya kazi kwa kukomoana........wanatafuta kila mwanya wa kupata rushwa......

Fuata muongozo wa leseni yako mkuu....uwe makini maana wengine wanakuwaga matapeli.....kabla ya maongezi yoyote na mtu usiyemfahamu kwanza dai kitambulisho cha huyo mtu.....
Shida ni hawa watu wa halmashauri wanapokuja kuuliza leseni.... Utata upo hapo kwamba fremu moja leseni mbili
 
Tuseme TRA wanashindwa kukaa vizuri na watoa huduma hizo za uwakala kurahisisha mambo maana terms zao kama vile zinapingana.
Watu wa leseni ndio wana matatizo sana, kwanza commission za wakala huwa zinakatwa kodi 10% kila mwezi lakini bado utaambiwa tena uombe leseni nyingine ya uwakala uilipie ada ya leseni na ukadiriwe kodi TRA yaani leseni 2 kwenye fremu moja ni haki kweli?
 
Kisheria Wako Sahihi. Leseni inalenga biashara na sio Premise.Hata hivyo kutegemea aina ya biashara ambazo unafanya unaweza kuomba aina flani za leseni ambazo ni more inclusive. Cha muhimu ni kuhakikisha kwamba aina ya biashara unayofanya inakuwa ndani ya leseni yako.
Asante, Leseni ipi kwa mfano inaweza include mfano biashara ya nguo na uwakala?
 
TRA hawahusiki na leseni za biashara, TRA wanahusika TIN Makadirio ya kodi nk..Wanaohusika na Leseni ni manispaa ya mji uliopo.
 
Shida ni hawa watu wa halmashauri wanapokuja kuuliza leseni.... Utata upo hapo kwamba fremu moja leseni mbili
Main Business hapo ni Ipi?Katika Biashara kunakuwa na Main Business.Ile Main Business ndo Inapaswa kuwa na leseni.Kama zote ni Main basi inabidi uwe na leseni.Mfano.Ukienda kwenye Maduka ya rejareja utakuta wanauza gas,na Mafuta taa lakini hawana leseni ya kuuza mafuta kutoka EWURA so ile sio main business na katika hali ya kawaida hutahitaji leseni.Ila kama unana zote zinakuingizia enough basi ni lazima uzilipie leseni ila kama ile ambayo sio main haikuingizii basi huna haja ya kuikatia leseni becoz sio main business yako.Sijui kama umenielewa kidgogo
 
Wenyewe wanadai hata kama sio main, as long as umeweka mabango na una operate basi lazima uikatie leseni.
 
Angalia kwenye Biashara yako,Kila ambacho kinakuingizia zaidi kati LESENI ya Main.Kile ambacho hakiingizi sana usikatie leseni.Hakikisha hata kwenye TAX reports zako ndicho unachotumia.Anapokuja mwambie na umweleze kwamba this is not my main business straight.Ukiona anakuzingu unamwambia utaangalia cha kufanya.usikubali watu wakuchoshe/Ila kama unaona Zote zinakulipa vizuri na kutoka vizuri basi katia zote leseni..Kuhusu compatibility ya Biashara na leseni hapo inabidi tujadili na kushauriana kulingana na ulipo na malengo yako na aina ya biashara
 
Back
Top Bottom