Leseni mpya za biashara mbona majanga

Leseni mpya za biashara mbona majanga

Kinyengeli

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
452
Reaction score
143
Habarini za kutwa wakuu, Kuna jamaa yangu maafisa biashara wamemkuta katika biashara yake akiwa hana leseni ya biashara, walipomuuliza akawajibu kwamba aliuliza kwa watu juu ya taratibu za kupata leseni ya biashara wakamwambia kuwa ili upate leseni ni lazima kwanza awe na nambari ya utambuzi wa mlipa kodi (TIN) kutoka TRA.
Akafunga safari mpaka TRA, maafisa wa TRA wakamwambia ili apate TIN ni lazima awe tayari kukadiliwa kodi stahili na alipie ndio wampe kibali akafate leseni Manispaa/Halmashauri husika, jamaa akakubali lakini wakasema hawawezi kumkadilia kodi bila kufika eneo la biashara ilipo, bahati mbaya biashara yake (Kiduka) kipo nje kidogo ya mji.
Baada kama ya wiki moja hivi ndio hao maafisa biashara wakapita kwaajili ya ukaguzi wa leseni, wakasema anafanya biashara bila leseni hivyo anatakiwa akalipe faini pamoja na maelezo yote hapo juu wakamng'ang'ania lazima alipe faini ya Tsh 50,000, bahati mbaya hakuwa na pesa wakati huo na gharama ya leseni ni Tsh 6,7000 hivyo awalipe Tsh 117,000 na akalipe bank. wakachukua baadhi ya bidhaa ili akazifate ofisini kwao endapo akienda kulipa na akichelewa mwezi mmoja gharama na faini itaongezeka.
Tusaidiane ushauri binafsi sijaona kosa lake je hapo kosa lake nini na ukizingatia biashara hivyo ndio kaianzisha mwezi huu?. Wao wanasema sheria inasema kabla ya kuanzisha biashara lazima kwanza uwe na leseni, wakati utaratibu wao huwezi kupata leseni ya biashara kama huna nambari ya mlipa kodi, na TRA hawawezi kukupa nambari bila kuja kukukadilia mapato, hapo mimi naona kuna namna ambayo kwa namna yoyote lazima mfanyabiashara ataonekana amevunja sheria hasa kwa kipindi ambacho atakuwa anasubiri kukadiliwa ni lazima afungue hiyo biashara yake, kama sio unyanyasaji kwa wananchi na kutengeneza mazingira ya rushwa nini? Tushirikishe nawewe huko uliko hali ikoje juu ya upatikanaji wa leseni mpya za biashara.
Nawasilisha.
 
kweli majanga. Tanzania kila kitu kigumu kupata. Mazingira rushwa lazima
 
Leseni muhimu,
ila hapo kwa tra kama vile huyo rafiki amedanganya,
tra wanakupa tin lazima wakutembelee.

Leseni ndio lazima utembelewe.
 
Ushauri wangu kwa wafanyabiasha wanaoanza na bila mtaji wa kutosha, jitahidini sana kuanza biashara zisizowalazimisha muwe na leseni. Piga deal mpaka mtaji ukue ndo utafute leseni na uanze kulipa kodi. Kama una mpango wa duka, anza kwa kupanga vitu mezani bidhaa nyingine acha nyumbani. Kwa kifupi, jifunzeni kukwepa kodi bila kuvunja sheria badala ya kusubiri 'utu' wa watu wa TRA.
 
mkuu, mimi nilifuata TIN TRA kabla ya kuanza biashara lakini niliwaambia mtaji nilionao na makadilio ya faida nitayopata, wakanipa TIN ndani ya siku 2. baada ya hapo nikaanza biashara na nikapeleka TIN halmashauri nikaambiwa nilipie form 15000/= na nikapata leseni siku hiyohiyo! binafsi ninajua sheria za kodi kwa kiasi cha kutosha! kama huyo jamaa bado atakuwa anatatizwa nichek pm au 0686822006 tusaidiane zaidi!
 
Back
Top Bottom