leseni ya duka la nyama ya mbwa.

tz1

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2011
Posts
2,121
Reaction score
536
Naomba msaada wa haya maswali,
Nataka kufungua duka la kuuza nyama ya mbwa.
1.Je inawezekana kupata leseni ya biashara
2.Na waTz wataichukuliaje hii biashara?maana naamini hii nyama si haramu.
 
kupata utapata lakini ulishafikilia wateja wako ni kina nani? na je utaliweka maeneo gani hilo bucha lako?
 
kupata utapata lakini ulishafikilia wateja wako ni kina nani? na je utaliweka maeneo gani hilo bucha lako?
Wateja na uhakika nitapata wazawa na wageni wakutoka bara la asia.
Nafikiria kuweka kwenye shoping centre hapa dar labda badaye na nyanda za juu.
Nashukuru kwa mchango wako.
 
Wateja na uhakika nitapata wazawa na wageni wakutoka bara la asia.
Nafikiria kuweka kwenye shoping centre hapa dar labda badaye na nyanda za juu.
Nashukuru kwa mchango wako.

Mkuu nimeipenda plan yako. Hapo mi naona ishu ni leseni maana wateja sio ishu. Na ukiingia kwa gia ya vyakula vya asili, utapata wahehe kibao.
 
Reactions: tz1
NYAMA HARAM!punda hacheui hana kwato 2,simba,nyani,chui,paka yani carnivorous wote haram
 
..Godfrey Sanga amehukumiwa kwenda jela kifungo cha miaka mitano baada ya mahakama kuthibitisha kuwa julai 7 alichinja mbwa wanne na kuwauza katika klabu ya pombe za kienyeji iitwayo TUPENDANE,kijana huyo pia amekiri mbele ya mahakama hiyo ya mkoni njombe kuwa si mara ya kwanza kwake yeye kuuza nyama ya mbwa na mara nyingine huwa anachuna mizoga iliyokufa na kuanza kuichuna ngozi na pia kuuza nyama kilabuni hapo,
sosi:RFA
NB:kama hili limetokea njombe,basi tuwe makini na mahali popote,huyu jamaa hayupo peke yake,niliwah kuleta bandiko hapa kuwa kuna jamaa hapo magomeni alikamatwa kwa tabia ya kuuza kuku waliokufa
 
Nyama itachinjwa kihalali na nitafuata taratibu zote za afya.
 
Nijuavyo mimi, mbwa anakula nyama za mifugo mingi tu kama nyama ya ng'ombe, mbuzi, kitimoto etc. Kwa hiyo kufungua duka la nyama ya mbwa inawezekana tu, kwani mtu akinunua nyama ya ng'ombe, mbuzi, kitimoto etc atajua mwenyewe akawape mbwa wake au ale mwenyewe
 
Reactions: tz1
Wateja na uhakika nitapata wazawa na wageni wakutoka bara la asia.
Nafikiria kuweka kwenye shoping centre hapa dar labda badaye na nyanda za juu.
Nashukuru kwa mchango wako.

Pia tengeneza vipeperushi na kuwagawia katika maduka yao a sehemu zao NYINGI za biashara!!! Ukiweza kuanza moja kwa moja na HOME DELIVERY service utawapata wengi zaidi maana haitokuwa na ulazima wa kuja kwako kufuata MBOGA; WEWE UTAFIKISHA MBOGA KWA MLAJI MOJA KWA MOJA
 
Reactions: tz1
Wasiwasi wangu ni Je? Mabwana Nyama wetu wanao ujuzi wakupima ze dog kwa ajili ya public use?
 
Reactions: tz1
Nashukuru kwa ushauri wako nitaufanyia kazi.
 
wateja wako wa kwanza watakuwa wenye vibanda vya chipsi na mishikaki. Mabucha hayo yakienea na nyama ya mbwa ikiwa cheaper kuliko ng'ombe, tutalishana sana mbwa kwenye mishikaki!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…