Lakini kwa sababu zisizojulikana awamu iliyopita ilimyima Leseni na badala yake wakapewa Vodacom.
sasa kati ya mengi na voda nani ana experience zaidi ya hii sekta?
Mengi angepewa ingekuwa ni njia nzuri ya kuinua wawekezaji wazalendo ambao wana mapenzi na machungu na nchi. Wapo wengine ambao wanamdhania Mengi kama dalali anayesimamia mitaji ya wakubwa wa nje huku yeye akijitapa kama ndie mwekezaji halali. Lakini yote katika yote ndio hivyo Mengi ni kipenzi cha Tanzania.
Kuna fununu kuwa mfanya biashara maarufu Bw. Reginald Mengi alikuwa wa kwanza kuomba leseni ya Mobile Telecommunication.
Lakini kwa sababu zisizojulikana awamu iliyopita ilimyima Leseni na badala yake wakapewa Vodacom.
Je kuna mtu anafahamu ukweli wowote kwenye fununu hii?
Je kama Mengi angepewa, ingekuwa ina impact gani katika uchumi wa nchi?
Je kuna specific number ya operators wa telecom ambayo TCRA wanataka tuwe nayo? Celtel ilikuja baada ya vodacom kama sikosei. Kama nafasi tayari zilikuwa zimejaa (sababu unayotaka tuamini ilifanya RM anyimwe/akose leseni) ilikuwaje celtel wakapata? Kuna wengine karibu wanne nasikia pia wapo mbioni kutoa telecom services (eg Excellent Telecom - HITS etc). Je hili linaweza kutupa mwanga ni kwa nini RM alikosa/alinyimwa leseni?
mheshimiwa tcra ndo kwanza ilikuwa imeundwa na ilikuwa hajawa as organised as it is now..back in 1999 when vodacom came in serikali had a long hand and influence on who gets those licenses!! watu kwenye telecoms wanajua mengi alibaniwa hii sio siri..uliza insiders pale tcra wakwambia..fanyeni utafiti!! and btw the telecoms business has nothing to do with your experience in telecoms especiallu local shareholders..na ukiwa una business ya kuuza kuku u can bring a telecoms company in and register and follow procedures za tcra..manji . caspian wanajua nini hukusu telecoms??
Naanza kusikia Harufu ya Mengism humu ndani. yaani jamaa anashindwa kufuata vigezo, akipigwa chini anaanza kulia lia naonewa na nyie mnakurupuka na kucheza ngoma teheee