OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Ni katika muendelezo wa mjadala, ndugu Justine Kakoko, alisema wasio na hela watakuwa atika hali mbaya ya kuweza kuongea.
Hapa alizingatia kuwa maudhui ni picha, mawazo, maoni, elimu na chochote ambacho mtu ataweka mtandaoni, Kifupi ni kuwa ili uongee kwa uhuru ni lazima uwe na leseni kwa hiyo wasio kuwa na hela hawataweza kumiliki leseni na maana yake mawazo yao watayatoa wakiwa bafuni wanaoga.
Swala hili aliweka wazi kuwa ni kinyume cha Katiba ambayo ina mapa uhuru raia kutoa mawazo yake kwa uhuru.
Kwa gap kama hili, itakuwa shida sana kwa watu masikini kuibukia utajiri kupitia mitandao ya kijamii kama bahati iliyomkuta Piere Gumbo, au yule mtoto aliyekuwa anaimba kule Dodoma, mbaya zaidi ni kwa wale wasanii wanorekodi teasers ili kupata walau wadhamini mtandaoni.
Pia kuna vijana masikini wanaofanya komedi ambao wengi wameibukia kupitia mitandao ya kijamii, yaani ili ufikiri vizuri mfikirie Dullvani, Oka Martin, Carpoza, Mkali wenu na wengineo ambao kupitia maudhui ya mtandaoni wamepata kujulikana na kujiajili.
Kwa hiyo basi hili swala la mwenye hela ndio atakuwa na uhuru wa kuongea, litafanya hata uwezo wa kujiajiri kupitia mitandao ya kijamii upungue kwa kuwa masikini hawatakuwa na namna ya kuwasilisha ubunifu wao wa kisanaa au uhuru wa kuzungumza kwenye mitandao ya kijamii.
Naendelea kutoa hoja kidogo kidogo zilizojhadiliwa katika kikao huru cha mjadala kilichofanyika Agosti 15, 2020.
Signed
Oedipus