Samedi Amba LLC
Member
- Apr 5, 2024
- 81
- 117
Habari wanaJF,
Ni mimi tena. Nimekaa nje siku nyingi sijapost, lakini nimerudi tena mchezoni. Changamoto za hapa na pale, lakini nothing that I couldn't handle, by God's grace (hakuna kisichoshindikana kwa Mungu).
Nimekuwa na threads kadhaa kuhusu Upwork hapo nyuma. Kwa imani kuwa platform ina msaada kwa wengi wanaoanza maisha ya freelancing (au ambao wanatafuta wateja humo).
www.jamiiforums.com
www.jamiiforums.com
Awali tulizungimzia namna ya kuapply kazi Upwork, na mbinu chache hivi. Leo ngoja tuzungumzie wateja.
Kuna mtu humu aliwahi kusema "no sales, no business".
Nakubaliana naye. Mteja, na huduma kwa wateja, ndo kitovu cha mafanikio mtandaoni. Hebu tuzungumze kidogo kuhusu wateja hawa, jinsi ya kuwapata, na jinsi ya kuwatunza.
Naassume kwamba kufikia sasa, umekamilisha CV wako, na una nguvu mpya.
Unataka wateja ambao:
1. Tafuta Kazi
Kuna kitufe kinajiita "Find Work" kule Upwork. kinafanana hivi:
Ukikibonyeza, utaona kazi kibao zimejipanga. Angalia mfano unaofuata:
Sasa, itabidi uelewe namna ya kuchekecha mkeka hapa, maana kufikia hapa watu wengi hukata tamaa. Nifuate nikuonyeshe cha kufanya...
2. Anza Kusoma dalili za Mteja anayemaanisha
Unakumbuka tulichokizungumza awali? Narudia. Unahitaji mteja ambaye:
Ishara #1: Tafuta Reviews za Nyota tano (5-star reviews)
Hii ishara inaonyesha kuwa watu wengi wamefanya kazi na mteja huyo na wanaridhia mahusiano mazuri waliojenga naye.
Hamna shida ukijaribu kufanya kazi na wateja mbalimbali wapya. Changamoto ni kuwa watu kama hao hawafahamiki, na huwezi kujua utapata uzoefu gani kwake.
Tafuta ishara kama ifuayavyo:
Weka mouse yako juu ya star ratings zake ili kuona details zaidi kuhusu nyota zake tano:
Ishara #2: Je, Ametumia Gharama Upwork?
Mteja anayelipa vizuri lazima awe mtoaji pia (inashuhudiwa kwa pesa alizotumia kwa kazi zake mbalimbali hapo awali). Mteja mzuri ana pesa za kuajiri watu na kuwalipa vizuri.
Kwa mfano, huyu jamaa hapa chini ametumia zaidi ya dola 30,000 katika kazi zake. Tafuta watu kama hao:
Ishara #3: Rate Card (Anavyolipa kwa kazi kwa saa)
Kiswahili kigumu. Lakini nnachomaanisha hapa ni kuwa mteja mzuri analipa vizuri kwa kila saa ya kazi. Wenzetu ughaibuni huthamini muda wa kazi, kwa hiyo kila saa inashughulikiwa na kulipiwa.
Kwa mfano, ukiwa unatafuta mtu anayelipa $15 kwa saa, unaweza kumtafuta jamaa kama huyu:
Ishara #4: Ofa za Muda Mrefu
Kuna wakati utataka kufanya kazi na watu ambao unaweza kuwa nao kwa muda mrefu. Kwa mfano, ukilipwa $15 kwa saa, masaa 8 kwa siku, siku 5 za wiki, ni sawa na $600 kwa wiki, $2400 kwa mwezi (Tshs. 6M kwa mwezi). Mtu kama huyo ukifanya naye kazi hata kwa miaka miwili... Unanisoma.
Utahitaji kuwa na skills za kutafuta, kupata na kutunza wateja kama hawa kwa muda mrefu. Assumption ni kwamba mpaka hapa mtakuwa mnafanya kazi vizuri.
Tafuta tafuta maneno kama "long term" ili kugundua wateja kama hawa. Angalia pia na muda wa mkataba:
Endelea kutafuta kazi kadhaa kama hizi. Kuna raha kuwa wa mteja anayekuthamini nawe ukampa your very best kikazi. Kuna ishara nyingine zinazoambatana na hili, kama vile:
Ishara #5: Mteja ana Siku Nyingi Upwork
Kwa hili, ni vyema kuepukana na mteja aliyeingia Upwork majuzi. Information hii utapata kwa kuangalia sidebar ya kulia, kama ilivyoonyeshwa kwenye picha iliyopo hapo chini:
Mpaka sasa umeanza kuelewa nondo zitakazokupa ushindi. Tuendelee na ishara zingine.
Ishara #6: Uzoefu wa Waliofanya naye kazi hapo awali
Kuna haja ya kuangalia feedback ya waliotangulia. Itakusaidia kubaini mbivu na mbichi.
Mrejesho wa kuridhisha ni ishara tosha ya mteja mzuri. Ishara nyingine ni pamoja na
Ishara #7: Zingatia anavyomlipa mfanyakazi mmoja mmoja
Picha ya hapo juu ni mfano wa mteja anayelipa mjasiriamali mmoja $1,296 na mwingine $426. Kuna uhakika wa kupata walau $1,000 kwa mteja kama huyu.
Tanua malengo. Unaweza kutafuta wateja wanaolipa $10,000 kuendelea. Maana wapo (kuna mteja aliwahi kunilipa $30,000 ndani ya miezi michache, kwa hiyo nafahamu).
Wateja kama hawa wanapenda "personalization". Kwa mfano, mwite kwa jina lake la kwanza unapotuma ombi la kazi. "Hi Jane" ni bora kuliko "Hi" tu.
Ishara #8: Wateja kama hawa huwapa wafanyakazi mrejesho mzuri (Hadi nyota 5)
Kuna wateja ambao husahau/kupotezea mrejesho baada ya kazi nzuri. Ili kufanikiwa Upwork, unahitaji mrejesho mzuri. Tafuta mteja anayezitoa:
3. Unapotafuta kazi, fungua kila kazi kwenye tab yake
Usitumie dakika mbili kutafuta kazi. Chukua muda wa kutosha (lisali moja kuendelea) kupata wateja wanaoendana na huduma unayoweza kutoa.
Kuwa huru kufungua tabs zinazozidi ishirini. Wanasema tafuta utaona.
Wateja wazuri wapo, ila inabidi uwatafute. Ukifikia mwisho wa list, bonyeza kitufe cha Load More Jobs kuendelea.
Usiogope kuapply kazi ambazo zimekuwa posted hadi masaa 8 yaliyopita. (Baadaye ntakuja kuleta Uzi ambao unakuwezesha kupokea notification za kazi mpya kwa njia ya Message, Slack na Email).
4. Angalia kazi zilizopo, kisha chagua kazi unayoipenda
Ushachagua kazi 30 kuendelea. Usipoteze muda kujaribu kuapply kila kazi. Angalia kinachokufaa. Utajua kazi ambayo unaweza kufanya kwa ubora. Ichague ili uendelee.
Homework (Kazi ya Ziada)
Mpaka sasa, unajua namna ya kuapply kazi Upwork. Sasa, fanya hivi:
Ni mimi tena. Nimekaa nje siku nyingi sijapost, lakini nimerudi tena mchezoni. Changamoto za hapa na pale, lakini nothing that I couldn't handle, by God's grace (hakuna kisichoshindikana kwa Mungu).
Nimekuwa na threads kadhaa kuhusu Upwork hapo nyuma. Kwa imani kuwa platform ina msaada kwa wengi wanaoanza maisha ya freelancing (au ambao wanatafuta wateja humo).
Hayawi hayawi, hua. (Kozi ya Upwork ipo jikoni)
Habari wanaJF, Ni mimi tena, na natumaini kuwa upo vizuri unaposoma maneno haya. Leo imekuwa siku ya Idd kwa ndugu zangu waislamu, na wasabato fulani wapo kwenye msimu wa makambi. Yote mema.... Ee bwana, juzi kati nilizungumzia kozi yangu ya Upwork nitakayoitafsiri kwa ajili ya kusaidia...
Nafikiria kuleta kozi hapa jinsi ya ku-apply na kutoboa Upwork. Lakini naomba tusemezane kwanza...
Habari wanaJF, Ni mimi tena (It's me again). katika pita pita zangu, nimeangukia kozi moja makini ambayo naweza kuileta kwenu kwa ajili ya kusaidia wanaotaka kufanya kazi Upwork. Nina account huko, na nimefanikiwa pakubwa. Kozi screenshot yake hii hapa: Niliipata kwa mKenya fulani hivi...
Awali tulizungimzia namna ya kuapply kazi Upwork, na mbinu chache hivi. Leo ngoja tuzungumzie wateja.
Kuna mtu humu aliwahi kusema "no sales, no business".
Nakubaliana naye. Mteja, na huduma kwa wateja, ndo kitovu cha mafanikio mtandaoni. Hebu tuzungumze kidogo kuhusu wateja hawa, jinsi ya kuwapata, na jinsi ya kuwatunza.
Naassume kwamba kufikia sasa, umekamilisha CV wako, na una nguvu mpya.
Unataka wateja ambao:
- Wanalipa vizuri
- Ni rahisi kufanya naye kazi
- Wamekuwa vetted (wanafanya kazi kihalali. Epuka matapeli!)
- Wanaonyesha nia ya kufanya kazi na wewe kwa muda mrefu
- Watakupa star rating ya nyota tano
1. Tafuta Kazi
Kuna kitufe kinajiita "Find Work" kule Upwork. kinafanana hivi:
Ukikibonyeza, utaona kazi kibao zimejipanga. Angalia mfano unaofuata:
Sasa, itabidi uelewe namna ya kuchekecha mkeka hapa, maana kufikia hapa watu wengi hukata tamaa. Nifuate nikuonyeshe cha kufanya...
2. Anza Kusoma dalili za Mteja anayemaanisha
Unakumbuka tulichokizungumza awali? Narudia. Unahitaji mteja ambaye:
- Analipa vizuri
- Ni rahisi kufanya naye kazi
- Amekuwa vetted (Epuka matapeli!)
- Anayeonyesha nia ya kufanya kazi na wewe kwa muda mrefu
- Ambaye atakupa star rating ya nyota tano
Ishara #1: Tafuta Reviews za Nyota tano (5-star reviews)
Hii ishara inaonyesha kuwa watu wengi wamefanya kazi na mteja huyo na wanaridhia mahusiano mazuri waliojenga naye.
Hamna shida ukijaribu kufanya kazi na wateja mbalimbali wapya. Changamoto ni kuwa watu kama hao hawafahamiki, na huwezi kujua utapata uzoefu gani kwake.
Tafuta ishara kama ifuayavyo:
Weka mouse yako juu ya star ratings zake ili kuona details zaidi kuhusu nyota zake tano:
Ishara #2: Je, Ametumia Gharama Upwork?
Mteja anayelipa vizuri lazima awe mtoaji pia (inashuhudiwa kwa pesa alizotumia kwa kazi zake mbalimbali hapo awali). Mteja mzuri ana pesa za kuajiri watu na kuwalipa vizuri.
Kwa mfano, huyu jamaa hapa chini ametumia zaidi ya dola 30,000 katika kazi zake. Tafuta watu kama hao:
Ishara #3: Rate Card (Anavyolipa kwa kazi kwa saa)
Kiswahili kigumu. Lakini nnachomaanisha hapa ni kuwa mteja mzuri analipa vizuri kwa kila saa ya kazi. Wenzetu ughaibuni huthamini muda wa kazi, kwa hiyo kila saa inashughulikiwa na kulipiwa.
Kwa mfano, ukiwa unatafuta mtu anayelipa $15 kwa saa, unaweza kumtafuta jamaa kama huyu:
Ishara #4: Ofa za Muda Mrefu
Kuna wakati utataka kufanya kazi na watu ambao unaweza kuwa nao kwa muda mrefu. Kwa mfano, ukilipwa $15 kwa saa, masaa 8 kwa siku, siku 5 za wiki, ni sawa na $600 kwa wiki, $2400 kwa mwezi (Tshs. 6M kwa mwezi). Mtu kama huyo ukifanya naye kazi hata kwa miaka miwili... Unanisoma.
Utahitaji kuwa na skills za kutafuta, kupata na kutunza wateja kama hawa kwa muda mrefu. Assumption ni kwamba mpaka hapa mtakuwa mnafanya kazi vizuri.
Tafuta tafuta maneno kama "long term" ili kugundua wateja kama hawa. Angalia pia na muda wa mkataba:
Endelea kutafuta kazi kadhaa kama hizi. Kuna raha kuwa wa mteja anayekuthamini nawe ukampa your very best kikazi. Kuna ishara nyingine zinazoambatana na hili, kama vile:
Ishara #5: Mteja ana Siku Nyingi Upwork
Kwa hili, ni vyema kuepukana na mteja aliyeingia Upwork majuzi. Information hii utapata kwa kuangalia sidebar ya kulia, kama ilivyoonyeshwa kwenye picha iliyopo hapo chini:
Mpaka sasa umeanza kuelewa nondo zitakazokupa ushindi. Tuendelee na ishara zingine.
Ishara #6: Uzoefu wa Waliofanya naye kazi hapo awali
Kuna haja ya kuangalia feedback ya waliotangulia. Itakusaidia kubaini mbivu na mbichi.
Mrejesho wa kuridhisha ni ishara tosha ya mteja mzuri. Ishara nyingine ni pamoja na
Ishara #7: Zingatia anavyomlipa mfanyakazi mmoja mmoja
Picha ya hapo juu ni mfano wa mteja anayelipa mjasiriamali mmoja $1,296 na mwingine $426. Kuna uhakika wa kupata walau $1,000 kwa mteja kama huyu.
Tanua malengo. Unaweza kutafuta wateja wanaolipa $10,000 kuendelea. Maana wapo (kuna mteja aliwahi kunilipa $30,000 ndani ya miezi michache, kwa hiyo nafahamu).
Wateja kama hawa wanapenda "personalization". Kwa mfano, mwite kwa jina lake la kwanza unapotuma ombi la kazi. "Hi Jane" ni bora kuliko "Hi" tu.
Ishara #8: Wateja kama hawa huwapa wafanyakazi mrejesho mzuri (Hadi nyota 5)
Kuna wateja ambao husahau/kupotezea mrejesho baada ya kazi nzuri. Ili kufanikiwa Upwork, unahitaji mrejesho mzuri. Tafuta mteja anayezitoa:
3. Unapotafuta kazi, fungua kila kazi kwenye tab yake
Usitumie dakika mbili kutafuta kazi. Chukua muda wa kutosha (lisali moja kuendelea) kupata wateja wanaoendana na huduma unayoweza kutoa.
Kuwa huru kufungua tabs zinazozidi ishirini. Wanasema tafuta utaona.
Wateja wazuri wapo, ila inabidi uwatafute. Ukifikia mwisho wa list, bonyeza kitufe cha Load More Jobs kuendelea.
Usiogope kuapply kazi ambazo zimekuwa posted hadi masaa 8 yaliyopita. (Baadaye ntakuja kuleta Uzi ambao unakuwezesha kupokea notification za kazi mpya kwa njia ya Message, Slack na Email).
4. Angalia kazi zilizopo, kisha chagua kazi unayoipenda
Ushachagua kazi 30 kuendelea. Usipoteze muda kujaribu kuapply kila kazi. Angalia kinachokufaa. Utajua kazi ambayo unaweza kufanya kwa ubora. Ichague ili uendelee.
Homework (Kazi ya Ziada)
Mpaka sasa, unajua namna ya kuapply kazi Upwork. Sasa, fanya hivi:
- Tafuta walau kazi 20 unazozipenda Upwork
- Nitumie kazi uliyoichagua (link ya kazi hiyo ya Upwork), kupitia themastaklass@gmail.com, au tumaDM (hii inaweza kuchelewa kidogo), au nitafute WhatsApp kupitia +255742308110.