Naomba mtupokee, katika forum yenu, tunatambua kutakuwa na hoja nyingi kutuhusu na sisi tupo hapa kwa ajili ya hilo, tutajitahidi kadiri tuwezavyo kuwapatia majibu sahihi.
Karibu sana JF...kama kweli wewe ni mwakilishi wa Starmedia, basi tambua ya kwamba ninyi ni matapeli tu wala hamna nia nyingine zaidi ya hiyo.
Mna propaganda za kinyonyaji na zilianza kudhihirika tokea mnaanza kufanya recruitment.
QoS zenu ni mbovu hakuna mfanowe na mbaya zaidi teknolojia yenu haikidhi kabisa kiu ya watazamaji.