Binafsi naona sababu kubwa ni mwendelezo wa mapokeo ya asili toka kuumbwa kwa mwanadamu (Mwanzo mungu alimuumba adamu-kupitia yeye mwanamke akapatikana). Hivyo mapokeo ya mila na desturi zetu toka enzi za mababu na kumbuka tamaduni hudumishwa kwa kuendelezwa kizazi hadi kizazi ndio maana jamii zilizo nyingi huamini kuwa mwanaume ndiye anakuwa wa kwanza kuonyesha hisia ya upendo kwa mwanamke.
Kuhusu kuonekana malaya.....mh naona ni mtazamo binafsi tu!, ila naona wanawake wengi wanakosa nguvu ya uthubutu ya kum-face mwanaume na kumwambia la moyoni (kama amemzimia) na hicho ndicho naona mungu amewanyima wanawake.