Let's talk about savings: Ikitokea umeachishwa/umeacha kazi leo, una akiba ya kukutosha kwa siku ngapi?

Mimi nina miezi 4 sasa sijaweka akiba,mwaka huu tika umeanza nlikuwa na majukumu fulani yamenifanya nishindwe kuweka akiba
 
Ila honestly speaking,kusave ni mtihani jamani,sikumbuki mara ya mwisho mishahara yangu kukutana,hata 5000 🙁🙁🙁
 
Binafsi kila nikipata hela yangu ya mshahara naweka savings kabla sijautumia

250,000 ndo akiba nayoiweka kwa mwez! Kwahyo ninayobaki nayo ni ndiyo napanga nayo budget!

Mwaka ujao nina plan za kuongeza kiwango cha kusave maana nauhakika naweza anza mradi wakunipatia kipato cha ziada kuliko kutegemea kale ka mwisho wa mwez
 
Aiseee,, ngoja ntajaribu hiyo ya kuwaambia benki wakate juu kwa juu
 
Huwezi kusave pesa bila kuwa na mpango maalumu,hii ndo unajikuta umesave 3months,ndani ya siku mbili unakuta saving yote umeimaliza.
Saving inanoga endapo unalengo maalumu/mahususi vinginevyo hamna saving.
 
Hakuna pesa itakutosha. Mungu tu akupe neema ya kukuinulia watu.
 
mimi nilianza kazi miaka miwili nyuma nikawa natumbua sana ,ila kama minne nyuma nikagunduka kwamba haya sio maisha ,

ni miezi mitano kama hivi nikaanza kusave wakuu huwezi amini mwiki mbili nyuma nikawa na kiasi cha milioni moja na saivi nimenunua kiwanja tayari na nafanya mpango ndani ya mwaka huu niwe na viwanja kama viwili hivi kisha mwakani niwe na viwanja viwili tena jumla vinne kwa uwezo wa mungu..

kisha hapo naanza kufikiria biashara ya kufanya ,
 
Safi sana mkuu, unatupa moyo na sie wengine kuona kua mambo yanawezekana kama hutojali kwa upande wa changamoto katika suala la saving ipi ilikupata na ulipigana vipi kuishinda mana kwangu changamoto ni kua na save lakini shida inapopiga hodi hua ni majanga inakomba hela yote naanza na moja sasa sijajua kua tatizo ni amount ninayo save ni ndogo (kulingana na kipato changu) mpaka saving yangu inashindwa kuhimili changamoto za kiuchumi mara zitokeapo au nini? (i don't know) Na je, mwenzangu ulikua unatumia njia gani ku save kwa kuweka bank (saving acc) au ulifungua fixed acc special for saving only? Au kuweka m-pawa kama njia ninayoitumia mimi?
 

lita kumi mwaka mzima, unatania wewe labda kama upo peke yako
 
I' m not believing in savings rather I am believing in adding new investment
 
Jiulize kwanini wakina Mark Zuckerbeg mmiliki wa facebook anarudia nguo? ya jana anavaa leo pia na ni milionia? Matumizi yasio ya lazima ndio yanatukosti wengi, jaribu fanya hivi. Weka malengo unataka kufanya nini, akili yako iweke kwenye malengo yako na usitetereke, Weka akiba na kitakachobaki ndio utumie na sio unatumia na kinachobaki ndio unaweka akiba, Tumia muda mwingi kwenye kazi, wachina wanafanikiwa kwa sababu wanalala masaa machache sana muda wote ni kazi tu. Mama mmoja wa kichina anamiliki duka kariakoo mchana kutwa yupo dukani usiku anafanya kazi kama massage therapist hoteli flani kubwa hadi saba usiku, kwa siku anapumzika masaa 6 tu. Nakumbuka kipindi nafanya kazi posta kuna msichana mmoja kazi yake ni office attendance. Akitoka hapo office saa kumi na moja mbio anakimbilia kariakoo ananunua mzigo wa viatu vya bei rahisi kwa jumla anamwaga chini kwenye kiroba anauza. Anafanya kazi mpaka saa tatu usiku ndio anarudi nyumbani, alianza na mtaji wa elfu 50. Sasa amekodi majiko kwenye Bar mbili tofauti, yupo mbali sana
 
Hichi ulichokisema hapa niliwahi kukifikiria na kubadili kabisa kuwaza watoto wangu wawe nani, yani daktari, mwanasheria n.k, nitawapitisha njia itakayowafanya wajiajiri waachane na kuajiriwa kabisa wala wasiwaze.
 
Njia mojawapo ninayoitumia mimi nikufungua fixed account, uzuri wa hii njia unapata pesa zaidi ya ulioiweka kupitia interest rate.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…