Letter from death row inmate to his mother

Letter from death row inmate to his mother

Abunwasi

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2009
Posts
5,486
Reaction score
3,473
A prison inmate on death row soon to be put on the electric chair was asked his last wish before he died, He asked for a pen and paper and wrote:-

✍Dear Mum,
If the law was fair, today you could be here with me waiting to be hanged together in the electric chair, but since the law is so blind, I have been convicted for the crimes we committed together, Mum, remember how it started.

Do you remember the day I stole my friends sweet, you didn't punish me, you only said I was young, Mum remember when I used to steal dad's money but you didn't report me, remember at 15 when I stole our neighbours bicycle i hid it in the garage you saw me and kept quite I was with you and later I sold it to scrap you did nothing.

Mum the day I was suspended from school for smoking and dodging lessons dad wanted to punish me but you stopped him, remember very well that day you had bitter argument with dad because you supported me saying that the teachers were wrong, and when me and my friends broke into Jimmy's shop did you call the police? Remember I was hidden at home.

Mum, you never guided me, I was just a child, a little young boy who needed your guidance but you loved me so much and never corrected me and now its your love that has made me to die of a shameless death in this electric chair being convicted for the crimes we committed together...

Your loving son.✍

To all parents out there... here is a big lesson for us, let's guide our children well, If your child does something wrong punish them, help them to choose well from good and bad, help them to learn, don't love so much to extent of spoiling children.
 
Ni makosa makubwa sana,kulea mtoto kwa kumdekeza.Kama unampenda,mlee mtoto wako katika njia ipasayo.Nae hataiacha hata atakapokuwa mzee.
 
kweli wapo wamama wanawaharibu watoto wao kwa mapenzi yaliyopitiliza....japo si kwa kiingereza
 
Well, some individuals never mature and they continue to do the wrong things till death takes them a part!!!
 
Huyo badala ya kuungama na kujisamehe anamlaumu mama yake wakati maandishi yake yanaonyesha alikuwa anajua aliyokuwa akiyafanya yalikuwa ni makosa! Aliamua kwa utashi wake kufuata tamaa zake na kudharau maonyo ya baba yake. Mbona hakumwandikia baba yake?
 
Huyo badala ya kuungama na kujisamehe anamlaumu mama yake wakati maandishi yake yanaonyesha alikuwa anajua aliyokuwa akiyafanya yalikuwa ni makosa! Aliamua kwa utashi wake kufuata tamaa zake na kudharau maonyo ya baba yake. Mbona hakumwandikia baba yake?
Story za mitandaoni hizo ndugu usichukulia serious saaaana!
 
Huyo akalie tu hicho kiti.. Aache kulia lia
 
MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO
Hebu soma makala ya Mzee Stephen Maina [23-Jul-2013] nimeutoa kama ulivyo ili uelewe vizuri zaidi sababu ya kuleta ule uzi.

"Kichwa cha makala hii kinajieleza chenyewe. Katika makala yangu ya mwisho, nilitoa ufafanuzi wa mambo muhimu ambayo yatawasaidia wazazi na walezi kutoa misingi bora kwa watoto wao ili kuwaandaa kiakili, kimwili na kimaadili.

Jambo la msingi ni mazingira watoto wanamozaliwa na kuishi. Kwa kuwa baba na mama ndiyo wanaohusika baada ya kuzaliwa kwa mtoto, wao wenyewe ni msingi bora wa malezi.

Niliwahi kunukuu utafiti uliofanyika Uingereza na kubainisha kuwa mtoto awapo tumboni anaathirika na matendo anayofanya mama yake.

Kama mama ana huzuni au furaha, mtoto tumboni naye huathirika na mazingira hayo. Kwa maana hiyo, wazazi wanatakiwa kuishi kwa amani na upendo ili mtoto azaliwapo aweze kujengeka na kuwa na misingi bora.

Mara mtoto anapozaliwa anatakiwa kulelewa katika mazingira ya amani na upendo. Pale pasipokuwa na amani, penye fujo na mapigano, mtoto hawezi kupata amani na hivyo hukua katika mazigira ya wasiwasi.

Amani ikitoweka ndani ya nyumba, wazazi nao hukosa mawasiliano mazuri na watoto wao hivyo kukosa amani na usalama. Wakati mwingine baba anaweza kutoka nyumbani mapema na kurudi usiku bila kufahamu kinachoendelea.

Wenye shughuli za aina hii ni wengi na nawashauri wajitahidi wapate muda wa kutosha kukaa pamoja kama familia zao na kuzungumza kwa pamoja. Mazoea ya aina hii humfanya mtoto awe na imani na wazazi wake.

Kinababa wasiwe na tabia ya kubaki vijiweni kucheza bao, karata au kuishia kwenye vilabu vya pombe ambavyo huwafanya warudi nyumbani kwao usiku wa manane, wazazi wa aina hii huwafanya watoto wakue wakiwa na malezi ya mama zao pekee.

Kwa maana hiyo malezi ya watoto hayahitaji chakula na mavazi peke yake, kitu kikubwa ni maadili mema.

Watoto washawishiwe kuzingatia mila na desturi zinazofaa. Kwa mfano mtoto azoeshwe kuwasalimia wakubwa na hata kuwahudumia wageni wanaofika nyumbani. Wasisitizwe kuwa na heshima kwa wakubwa siyo tu wazazi wao bali walimu na wengine wanaowafahamu.

Eneo jingine la kuwalea watoto ni katika imani. Wazazi wengi wamekulia katika imani za dini mbalimbali hivyo watoto walelewe katika imani za wazazi wao. Mafunzo ya imani za madhehebu ya dini huanzia nyumbani. Watoto wanajifunza kutoka kwa wazazi wao wanaposali asubuhi na jioni, kabla ya kula na baada ya kula.

Matendo ya kiimani yanamjengea mtoto na kumjali Muumba wake. Endapo wataasi imani yao watakapokuwa wakubwa hayo ni yao na mzazi hana lawama wala kitu cha kufanya kwani ameshatimiza wajibu wake.

Kwa maana hiyo watoto wafuatane na wazazi wao kwenda kwenye nyumba za ibada kama kanisani au misikitini ili kupata mawaidha kutoka kwa viongozi wa madhehebu wanayoamini wazazi wao. Huu ni wajibu ambao hatuna budi kuutekeleza.

Mafunzo mengine ni kuwazoesha watoto kuishi katika mazingira ya usafi kwa maana ya kunawa mikono kabla na baada ya kula. Chakula nacho kiwe katika mazingira ya usafi.

Hatuna budi kuwazoesha watoto wetu wajishughulisha ma kazi za nyumbani bila kujali jinsi zao kama ni wasichana au wavulana. Kuosha vyombo vya chakula, kufua nguo na kusafisha eneo la ndani na nje ya nyumba ni masuala ambayo kila mtoto anatakiwa kufanya.

Hizi ni tabia ambazo wazazi wanatakiwa kufuatilia kwani ni msingi wa maisha yao ya baadaye. Kwa kufanya kazi kwa vitendo ni njia pekee ya kumjenga mtoto kimaadili".
 
wazazi watarajiwa somo hilo, likamateni
 
A lesson to learn, about the way we raise our son & daughters...! Hope lesson learned.
 
Back
Top Bottom