Ndugu wana jukwaa,
Leo ni siku ya huzuni tunapopokea habari za kuondoka kwa mmoja wa magwiji wa kweli wa filamu za mapigano kutoka Hong Kong—
Leung Choi-sang.
Kwa wale tuliozaliwa na kukua tukitazama mikanda ya VHS na filamu za kusisimua za miaka ya 70 na 80, Leung hakuwa mwigizaji tu, bali alikuwa nembo ya ufundi na nidhamu ya kutoa vichapo heavy.
Kung Fu Hustle: Wengi tutamkumbuka kama
"The Beast"—yule mzee mfungwa mwenye nguvu za ajabu ambaye alitikisa hisia za watu alivyomnyoosha
Stephen Chow. Hili lilikuwa jukumu lake la kwanza kama adui (villain), na alitupa msisimko usiosahaulika.
Enzi za Bruce Lee: Alijipatia umaarufu kwa kuigiza kama Bruce Lee kwenye filamu ya
The Dragon Lives Again, na pia alihusika nyuma ya pazia kama mratibu wa mapigano (
choreographer) kwenye filamu ya
The Tattoo Connection pamoja na filamu zingine kadhaa.
Kazi Nyinginezo: Aling'ara katika filamu ni kama
My Kung-Fu 12 Kicks pamoja na
Magnificent Bodyguards akiwa na
Jackie Chan.
Baada ya kustaafu kwa muda mrefu, alirejea kwa kishindo na kutuonyesha kuwa "chuma ni chuma" hata kikiwa cha zamani. Mwaka 2020, alionekana kwa mara ya mwisho kwenye tamthilia ya
Heroes, akituachia urithi wa mwisho wa kipaji chake.
Sanaa yake ya mapigano, kasi yake, na uwezo wake wa kuchekesha na kutisha kwa wakati mmoja utabaki mioyoni mwetu daima. Tunapoteza mwalimu, mwigizaji, na shujaa wa kizazi chetu.
Lala salama, "The Beast." 🥋