Hali hii ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya pesa ya mali ya umma inatisha sana. Kinachosikitisha zaidi ni kuwa hata Ikulu inahusika kwenye hili.
Wakati huko Dodoma wanazozana kuhusu taarifa za CAG, Rais yuko angani muda wote akipasua anga kuanzia: UAE, India, Zambia, Rwanda na leo yuko Angola!. Pamoja na kuwa ni moja ya majukumu yake kama Rais kuwa na mahusiano na nchi za nje, najiuliza kwa nini hatumii ndege ya Rais iliyonunuliwa kwa ajili ya safari za Rais?
Ndege anayotumia sasa ni ndege mpya Boeing 737-9Max inayobeba abiria zaidi ya 170 yenye ratiba ya kwenda India. Wajumbe wanaoambatana na Rais kwa idadi hiyo huwa wanaenda kutalii au ofisi zao zimeamua kufanya kazi hata nje ya nchi?
Air Tanzania wanasifiwa kwa kutengeneza hasara, kama inawalipa vizuri sidhani kama kuna uadilifu hapo maana ATCL inawezesha ubadhirifu kwa kwenda kinyume na ratiba yake ya India. Matokeo yake tunaona Air Tanzania ikitumia Airbus 220-300 kwenda India wakati wahindi wanaolipia kusafiri kwa starehe ya Dreamliner waliwahi kulalamikia mabadiliko ya ndege kama haya.
Air Tanzania inapaswa kubaki kwenye reli kibiashara, kama wataruhusu siasa uchara kuingilia mipango ya kiufundi ya kampuni na ratiba zake zinazolipa kampuni itarudia historia mbaya ya nyuma.
Ndege kuunguza mafuta hadi mlango wa Red Sea na kurudi bila kutua na kubeba mzigo wowote huu ni ubadhirifu mwingine kama sio uhujumu uchumi.