Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Wito wa LHRC unaungana na wa Chama cha ACT-Wazalendo, kilichohoji maswali kadhaa, ikiwemo nani anayefanya matukio hayo huku kikitaka Jeshi la Polisi kuwasaka wahusika.
Kauli za wadau hao, zinakuja baada ya kupatikana kwa mwili wa Kibao, katika eneo la Ununio jijini Dar es Salaam akiwa ameuawa na uso wake ukiwa umejeruhiwa kiasi cha ndugu zake kushindwa kuutambua.
Mwili wa kibao, umekutwa katika hali hiyo siku moja baada ya kuripotiwa kuchukuliwa katika eneo la Tegeta, mbele ya Jengo la Kibo Complex, baada ya basi la alilokuwa amepanda, kuzuiwa na magari mawili.
Kutokana na tukio hilo, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimeisihi Serikali ifanye uchunguzi wa kina na haraka kubaini wahusika na wachukuliwe hatua.
Soma Pia:
- Mbowe: Ripoti ya Uchunguzi wa Kifo cha Mzee Kibao ikiwa tofauti na tulichoona tutaipinga
- Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Mbali na LHRC, Chama cha ACT-Wazalendo nacho, kimelaani tukio hilo, kikisema kunaongeza hofu juu ya usalama na amani na kuchafua imani iliyopo kwa wananchi.